Mbunge wa Ukonga, Eugen Mwaiposa akifafanua jambo wakati wa
mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, hivi karibuni kuhusu fedha
zilizoidhinishwa na serikali kiasi cha sh. bilioni 3.9 kwa ajili ya kukarabati barabara
za jimbo hilo ambazo ziliharibika kutokana na mvua kubwa zilizonyesha
mwanzoni mwa huu. Mbunge huyo ameiomba serikali kuharakisha utoaji wa fedha
hizo. Kushoto ni Katibu wa Mbunge, Khalfan Kondo. (Picha na Francis Dande)
Na Peter Mwenda
MBUNGE wa Jimbo la
Ukonga, Eugine Mwaiposa ameiomba Serikali kutoa haraka fedha iliyoidhinisha sh.
Bil. 3.9 kwa ajili kukarabati barabara za Jimbo la Ukonga ilizoharibiwa na mvua
Aprili mwaka huu.
Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana alisema fedha hizo zinahitajika haraka
ili kurudisha mawasiliano kati ya eneo moja kwenda jingine yaliyotenganishwa na
mvua hizo na kusababisha kupanda kwa gharama za huduma za jamii kaama vyakula
na usafiri.
Alisema Serikali
katika awamu ya kwanza ya ukarabati huo ilitoa fedha kutoka mfuko wa maafa
jumla ya Sh. bil. 1.5 zilizotumika kukarabati baadhi ya madaraja ambayo
yalikatika karibu maeneo yote ya jimbo hilo.
Mbunge Mwaiposa
alisema jimbo lake ni kati ya yale yaliyoharibiwa vibaya na mvua na mengi
kukosa kabisa mawasiliano kama vile barabara ya Chanika na Msongola kupitia
daraja la Mvuti, barabara ya Msongola kwenda Kivule na Kitunda kwenda Magole B
kupitia daraja la mto Mzinga.
Alisema barabara nyingine
ni kutoka Gonga la Mboto kwenda Ulongoni A na B ambapo madaraja mawili
yalibomolewa na barabara itokayo Ukonga kwenda Mongo la Ndege kupitia daraja la
Kinyerezi.
Mwaiposa alisema
pamoja na fedha hizo kutolewa lakini bado zipo barabara na madaraja mengine
ambayo hayajapata fedha kama vile barabara ya kutoka Kiltex kwenda Bangulo na
Kitunda kwenda Mwanagati.
Alisema barabara
nyingine ambazo hazikupata fedha lakini zimeombewa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ni kutoka Chanika kwenda
Machimbo, Kivule kwenda mto Nyang'andu, Chanika Msumbiji kwenda Nzasa na
Kibeberu kwenda Magole.
Alisema wakati wa
uhakiki wa barabara zilizobomolewa na mvua zipo ambazo hazikutambuliwa
kuharibika kwake ambazo ni barabara ya Dunda yenye mita 2,000, Pugu Mpakani
mita 3,000, Barabara ya Mbondole Chanika na Yange Yange.
Mbunge huyo alisema
pamoja na juhudi za Serikali kutenga mafungu bado tatizo la miundombinu ya
barabara ni changamoto katika maeneo ya pembezoni ya Jiji la Dar es Salaam.
Alisema barabara hizo
zilitengenezwa zitasaidia kupunguza msongamano wa magari mengi kukimbilia
katika katika barabara kuu za jiji la Dar es Salaam.
Aliomba Serikali
ifungue milango kwa watu na makampuni binafsi kuwekeza kwenye barabara na
baadaye kutoza tozo kwa magari yanayotumia barabara hizo ili kuharakisha
maendeleo.

No comments:
Post a Comment