MKUU wa Mkoa wa
Tanga, Chiku Gallawa (pichani), anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika uzinduzi wa taasisi ya Handeni Kwetu Foundation,
utakaofanyika Jumanne ya Agosti 5, katika Ukumbi wa Vijana Social Hall,
Kinondoni, jijini Dar es
Salaam.
Tukio hilo la uzinduzi wa taasisi hiyo limepangwa kuanza saa
10 za jioni ambapo wamealikwa wageni mbalimbali kwa ajili ya kuitambulisha
kabla ya kuanza kazi zake rasmi nchini Tanzania.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msemaji wa taasisi
hiyo, Kambi Mbwana, alisema kuwa wameona wamualike RC Gallawa kuwa mgeni rasmi
kwakuwa ni miongoni mwa viongozi makini na wenye kiu ya maendeleo hapa nchini.
Alisema kuwa kitendo cha kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa Tanga,
kinaonyesha namna gani viongozi wa serikali wanashirikiana na wadau wote kwa
ajili ya kufanikisha mipango ya kimaendeleo.
“Tanzania imejaliwa kuwa na viongozi makini mno, hivyo
taasisi imemualika Mheshimiwa Gallawa kuwa mgeni wake rasmi ili ashirikiane na
wageni waalikwa kuitambulisha taasisi.
“Tunaamini kwa pamoja tutafanikisha kuitambulisha taasisi kwa
wadau wote, hususan Watanzania kwa kupitia Handeni Kwetu Foundation,
ukizingatia kuwa imesajiliwa kufanya kazi zake nchini nzima,” alisema.
Kwa mujibu wa Mbwana, sera na mikakati ya taasisi hiyo itaanikwa
katika utambulisho huo utakaokuwa na malengo mahususi ya kujikwamua kiuchumi na
kuhamasisha masuala ya utawala bora.
No comments:
Post a Comment