Jeshi la Polisi linaendelea kumshikilia na kumhoji aliyekuwa Mwakilishi
wa Jimbo la Kiembe Samaki (CCM), Mansoor Yussuf Himid (pichani), baada ya
kupatikana na silaha aina ya short gun yenye risasi zipatazo 112,
Bastola ikiwa na risasi 295 huku wakishikilia laptop yake.
Polisi
walifika nyumbani kwa Mansoor asubuhi na kupekuwa na kugundua vitu hivyo
baada ya kupata taarifa toka kwa wasamaria wema kuonesha wasiwasi wao
juu ya Mansoor.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo, Naibu Msaidizi
Mkuu wa Upelelezi Zanzibar Salum Msangi aliwaambia waandishi wa habari
kwamba pamoja na umiliki wa silaha hizo upo kisheria lakini anapaswa
kuwa na risasi za short gun 50 ambapo risasi za bastola kisheria
anatakiwa awe nazo 25 kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Risasi 5 zimetumika
polisi wanafuatilia zimetumika vipi. Mansour anakuwa ni kiongozi wa
kwanza katika historia ya Zanzibar kukutwa na kiasi kikubwa cha Risasi
zikiwa zimefichwa nyumbani kwake.
No comments:
Post a Comment