Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb
Abdul ‘Diamond Platinumz’ amesema yupo kwenye mazungumzo na muigizaji mkubwa
Nigeria ili aanze kufanya kazi na mpenzi wake ambaye pia ni muigizaji wa filamu
za Bongo, Wema Sepetu.
Awali Diamond alisema, kutokana na nafasi
aliyonayo yeye katika tasnia ya muziki anapenda naye mpenzi wake awe wa
kimataifa zaidi kupitia sanaa yake.
Akizungumza na Habari Mseto hivi karibuni,
Diamond alisema ameamua kufanya hivyo ili amsaidie mpenzi wake awe anafanya
kazi na wasanii ambao watamfanya afahamike Dunia nzima.
“Kwasababu nampenda na uwezo wa kumsaidia ninao
nimeamua kumsaidia, kuna msanii mmoja mkubwa wa Nigeria nimeanza mazungumzo
naye tumefikia pazuri tukimalizana tu wataanza kazi,” alisema.
Diamond kwasasa anatamba na kibao chake cha
‘Mdogo mdogo’ ambacho kinafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na
televisheni licha ya kuwa na kazi nyingi ambazo zilimtambulisha na kufanya
vizuri.
No comments:
Post a Comment