Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema),
akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa mashindano ya soka ya Mwidau CUP leo
mjini Pangani.
Na Mwandishi Wetu, Pangani
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), akiingia
uwanjani kuzindua mashindano ya Mwidau CUP .Kushoto ni mdahamini wa mashindano
hayo ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum Amina Mwidau.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), akiwa
ameshika ngao ya hisani ambayo iliwaniwa katika mchezo wa ufunguzi wa Mwidau
CUP, ambapo timu ya Torino iliibamiza APL ya Mwera bado 2-0
Na Mwandishi Wetu, Pangani
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amesema
hatua ya Tanzania kutofanya vizuri katika michenoa ya kimataifa ni kukosekana
misingi imara wa kuinua vipaji kuanzia ngazi ya chini.
Hayo alisema leo mjini Pangani alipokuwa akizindua
mashindano ya Mwidau CUP, ambapo asema hatua ya Tanzania kutoka patupu katika
mashindano ya Olimpiki ni kielelezo tosha cha kuhitaji maandalizi ya kina.
“Nchi yetu haijapata bahati ya kufanya vizuri kwenye michezo
kwani hivi juzi timu zetu zilikuwa katika michuano ya Olimpiki nchini Scotland
lakini hatukupata medani hata moja.
“Wiki iliyopita tulikuwa Maputo Msumbiji timu yetu ya Taifa
imetolewa kwenye mashindano ya Mataifa huru. Tanzania kwa mara ya mwisho ilishiriki
mashindano ya mataifa huru tangu mwaka 1980. Hatujawahi kushiriki tena na
sababu kubwa tumesahau kujenga vipaji,” alisema Zitto.
Alisema ni vigumu kumnenepesha ng’ombe siku ya moja ya
mnada ila kinachotakiwa ni juhudi kama zilizonzishwa na Mbunge wa Viti Maalum
Amina Mwidau (CUF), kuibua vipaji kuanzia ngazi za chini.
Alimtaka mbunge huyo kuhakikisha mashindani yajayo yakuwa
na timu za chini ya miaka 17 ambazo zinatasaidia katika kuibua vipaji zaidi.
“Hii itatusaidia kuwajua watoto bado wadogo kwani hapa
Pangani wapo kina Ulimwengu na kina Mbwana Samatta. Ninatoa wito kwa mashirika
ya umma kuwa na timu zao kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwani hii itasaidia
kuinua soka letu na hata michezo mingine katika Taifa letu,” alisema.
Kwa upande wake mbunge wa Viti Maalum, Amina Mwidau (CUF),
alisema mashindano ya mwaka huu yamekuwa na maboresho makubwa ambapo mshindi wa
kwanza atapata zawadi ya Sh 500,000 wa pili 400,000, wa tatu Sh 300,000.
No comments:
Post a Comment