HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 10, 2014

MO MUSIC: MAISHA YA USTAA NI SHIDA


Na Elizabeth John
BAADA ya kutamba na ngoma yake ya ‘Basi Nenda’, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Moshi Katemi ‘Mo Music’ amesema, staili ya maisha yake imebadilika kutokana na umaarufu alioupata.

Akizungumza na Habari Mseto kwa njia ya simu akiwa jijini Mwanza, Mo alisema kutokana na umaarufu alioupata kupitia wimbo huio imekuwa ni vigumu kutoka ndani na kuzunguka mtaani.

“Yaani maisha ya ustaa ni shida sana hasa usipoyazoea, unapotoka lazima ujue unapokwenda hakuna watu wengi usipokuwa makini inakuwa kero maana kila mtu atataka kukuangalia na kukusemesha,” alisema.

Alisema popote anapokwenda anatakiwa kuwa smati maana kila mmoja anamtazama yeye anafanya nini na yupo wapi.

Mo Music alisema kwasasa yupo kwenye mikakati ya kusambaza ngoma yake mpya ambayo yupo katika hatua za mwisho za uandaaji.

“Naomba wapenzi wangu wakae mkao wa kula nipo katika mikakati ya kutoa wimbo wangu mwingine, sipendi kuutaja jina kwasasa itakuwa ‘surprise’ kwa mashabiki wangu naomba wanipokee ;kama ilivyokuwa awali,” alisema nyota huyo.

No comments:

Post a Comment

Pages