HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 10, 2014

HAFSA KAZINJA AMTAJA 'MLALA NJE'

Na Elizabeth John
MSANII wa muziki wa kizazi kipya katika miondoko ya Zouk, Hafsa Kazinja ameachia video ya wimbo mpya ‘Mlala nje’ na kusambaza katika vituo mbalimbali vya televisheni.
 
Mwanadada huyo ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kupitia wimbo wake wa ‘Presha’ alioshirikiana vyema na Banana Zoro na kujijengea jina kubwa nchini.
 
Akizungumza Dar es Salaam jana, Hafsa alisema alipumzika kwa muda mrefu kwa ajili ya kujipanga ili kuendana na kasi ya muziki huo kwa 
sasa.
 
”Si kwamba nilikuwa kimya sana ila kuna wakati nilitoa wimbo wa 'Nuru' ambao nilishirikiana na Ali Kiba na ulifanya vizuri, lakini ujio huu wa sasa ni tofauti kidogo," alisema Hafsa.
 
Alisema video ya wimbo huo imetengenezwa na Mtayarishaji Meja huku ile ya kusikiliza 'audio' ameitengenezea kwa Mtayarishaji 69 na kwamba ana imani utafanya vizuri.
 
Alisema anapata imani hiyo kutokana na ujumbe uliopo kuwa ni tofauti na nyimbo zingine ambazo zipo sokoni kwa sasa na pia kuleta changamoto mpya katika fani hiyo.
 
Aliongeza video hiyo ipo tofauti na video zingine kutokana na jinsi alivyotengeneza na kikubwa angependa wasanii chipukizi kuiga mfano wake ili wafanye vizuri

No comments:

Post a Comment

Pages