MBUNGE wa
Jimbo la Iramba Mwigulu Nchemba na wa Temeke Abbas Mtemvu, wamesema kitendo cha
Yanga kutoshiriki michuano ya Kagame inayoendelea kutimua vumbi Mjini Kigali,
kunawapunguzia makali ya maandalizi ya ligi kuu na michuano ya Kimataifa.
Wabunge hao waliyasema hayo, wiki iliyopita katika tamasha
la Matumaini ambapo Wabunge wapenzi wa Yanga walipoumana na wenzao wapenzi wa
Simba na kuwalaza kwa mabao 3-2, katika mchezo uliopigwa dimba la Taifa Dar es
Salaam.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Nchemba alisema, kwa
muono wake mashindano hayo ni makubwa ambayo yangewapa mwanga Yanga wa
kujipanga zaidi kwa ajili ya msimu ujao, huku pia akilitupia lawama Baraza la
vyama vya Soka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA kwa kuwaondoa kisa
aina ya wachezaji ambao ilitaka kuwapeleka.
“Unajua Yanga wamefanya usajili na hao wachezaji waliokuwa
wakitakiwa kwenda uko, wamesajiliwa ndani ya Yanga, lakini kutokwenda kwao, ni
uzuni kwao kwani wangejipanga na kuona mapungufu kwa kuwa kuna timu kubwa
zinashiriki,”alisema Nchemba huku akimpongeza muandaaji wa tamasha la Matumaini
Erick Shigongo.
Naye Mtemvu, alisema, yeye kama mpenzi wa Yanga na ni mlezi
wa timu ya Wabunge wapenzi wa Yanga, hakupenda Yanga kutoshiriki katika
michuano hiyo, huku akisema kuwa labda Yanga uongozi na benchi lao wanajua
sababu za kutokwenda katika michuano muhimu kama hiyo.
“Mashindano yale ni mazuri, kwanza sisi wabunge
tumewafungulia kwa ushindi hivyo basi watashinda sana mechi zao, na pia
nampongeza Shigongo kwa kuandaa tamasha hili ambalo utukutanisha kila mwaka na
kutufanya tubadilishane mawazo,”alisema Mtemvu.
No comments:
Post a Comment