HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 23, 2014

JAJI MAKAME KUZIKWA LEO KIJIJINI KWAKE TONGWE MUHEZA, TANGA

Mke wa Jaji Lewis Makame, Marry Makame akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa mume wake, marehemu Jaji Lewis Makame  wakati wa kutoa heshimna za mwisho kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
 Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kushoto), Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick
 Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman.
 Picha ya Jaji Lewis Makame enzi za uhai wake.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa wasifu wa marehemu Jaji Lewis Makame wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam.
 Mke wa Jaji Lewis Makame, Marry Makame (katikati), akiwa na wanafamilia wengine wakati wa ibada ya kuaga mwili wa mume wake marehemu jaji Lewis Makame.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa pole kwa mtoto mkubwa wa marehemu Jaji Lewis Makame.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimpa pole Jaji Mkuu mstaafu, Jaji Augustino Ramadhani.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa pole kwa wafiwa.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitetea jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa na viongozi wa Serikali.
Wanafamilia wakiwa na huzuni.
Baadhi ya watoto wa marehemu.
Wanafamilia wakiongozwa na Jaji Mkuu mstaafu, Augustino Ramadhani kulia.



Na Mwandishi Wetu

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Lewis Makame anazikwa leo Kijijini Kwake Tongwe Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga.

Jaji Mstaafu Lewis Makame, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki.

Taifa limempoteza kiongozi muhimu aliyependa kutenda haki katika kazi zake za mahakama na aliyekuwa mwadilifu katika kutetea wengine alisema Mh: Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Alisema anaamini watu wanaomjua vizuri marehemu jaji Makame ni watenda maovu waliokuwa wakishtakiwa katika mahakama mbalimbali kwani alikuwa na uwezo mkubwa wa kusikiliza kesi zao na kuwatolea hukumu.

“Kwaniaba ya serikali na watanzania wote napenda kutoa pole kwa familia, pia napenda watu watambue kuwa jaji Makame aliweza kufanyakazi kwa ukamilifu wala hakuwa mbabaishaji alikuwa mmoja wa majaji wenye uzoefu mkubwa sana hapa nchini kwahiyo lipo pengo kubwa sana aliloliacha,” alisema

Naye aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Profesa Mwesiga Baregu alisema, jaji Makame alikuwa mmoja wa wazee wenye hekima, busara, uvumilivu na mwenye uwezo wa kuwasikiliza wengine.

“Uvumilivu wa jaji Makame katika kutenda kazi zake kumemsaidia kujua mambo mengi hivyo tunakili kuwa tumempoteza kiongozi muhimu na aliyekuwa shupavu, ila kwangu mimi naamini kuwa angeweza kutusaidia katika sakata hili la mchakato wa katiba mpya,” alisema

Jaji Makame alifariki dunia katika Hospitali ya AMI Trauma Center iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa leo katika kijiji cha Tongwe Muheza mkoani Tanga.

Aidha historia yake inaonesha kuwa Jaji Makame alikuwa na shahada ya kwanza ya sheria kutoka Chuo kikuu cha London nchini Uingereza ambako baada ya kufanya kazi nchini humo, alirejea nchini hapa na kulitumikia Taifa mpaka alipofikisha cheo cha Jaji wa Mahakama ya Rufaa.

Mbali na cheo hicho, Jaji Makame pia alikuwa Mwenyekiti wa NEC na mwenyekiti wa Jukwaa la Tume za Uchaguzi za Nchi Wanachama wa Jumuiya za Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-ECF).

1 comment:

Pages