Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu zoezi la kuwakamata watu wanaouza CD feki za kazi za wasanii.
Na Ramadhani Tembo
KAMPUNI ya Msama Promotions
kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo, imetangaza
neema kwa wasanii kwa kuanza zoezi la kuwakamata watu wanaouza nakala feki za
wasanii nchini.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo,
Alex Msama ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, zoezi hilo limeanza na
mpaka sasa wamekamata vijana wanne katika mkoa wa Dodoma na watatu mkoani
Mwanza.
Kuna kazi mbalimbali za wasanii
ambazo zinaibiwa kila kukicha huku wamiliki wa kazi hizo wakiendelea kushuka
kiuchumi na kutoona faida yoyote ya kazi hizo.
“Huu ni wakati kwa wasanii kunufaika na kazi
zao na tutahakikisha tutafika kila mahali hata sehemu zisizofikika kirahisi nah
ii yote ni kwea kujali kazi za wasanii”alisema Msama.
Alisema nakala zote zitakuwa
na stika za (TRA) kwa kuhakikisha hakuna wizi wowote unaotokea katika kazi
mbalimbali za wasanii.
Stika hizo zimewekwa ili
kuwabaini wale wote watakaobainika kuiba kazi za wasanii bila kujali wadhifa
wake wala cheo chake, na hili zoezi ni salam kwa yeyote anayetumia kazi za
wasanii bila kufuata utaratibu wa kisheria.
Pia alilipongeza jeshi la
polisi na wanashrikiana nalo na kuhakikisha zoezi hilo litakuwa endelevu na
watazunguka kila mkoa kuhakikisha kazi za wasanii zinaheshimiwa na zinalindwa
kwa.
No comments:
Post a Comment