Na Mwandishi Wetu
Shindano la Redd’s Miss Kinondoni, linazidi kushika kasi na kazi kubwa ipo leo wakati atakaposakwa mrembo mwenye kipaji kati ya 20 wanaoliwania taji hilo.
Shindano la Redd’s Miss Kinondoni, linazidi kushika kasi na kazi kubwa ipo leo wakati atakaposakwa mrembo mwenye kipaji kati ya 20 wanaoliwania taji hilo.
Mratibu wa Redd’s Miss
Kinondoni, Husna Maulid, alisema warembo hao wataanza mchakato wa kumsaka
Redd’s Miss Kinondoni Talent, katika shindano kali zaidi kuliko lote litakalofanyika
leo kwenye Ukumbi wa Maisha Club Uliopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Husna alisema, shindano
hilo la vipaji litakuwa la kipekee kutokana na mengine yote yaliyowahi
kufanyika na ana uhakika mkubwa watakaohudhuria watapata burudani ya aina yake.
“Kesho (leo) ni vipaji kwa
kwa sasa kinachosubiriwa ni siku tu na warembo 20 wapo katika mazoezi makali
kwa ajili ya shindano hilo.”
Shindano la Redd’s Miss
Kinondoni linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Escape 1 uliopo Mikocheni,
Dar es Salaam huku kukiwa na burudani kali toka Malaika Band inayoongozwa na
Christian Bella.
Taji la Redd’s Miss
Kinondoni kwa sasa linashikiliwa na Lucy Tomeka, ambaye naye alivikwa na
aliyekuwa Redd’s Miss Tanzania, Brigitte Alfred.
Warembo wanaoshiriki
shindano hilo wanatoka vitongoji vya Sinza, Msasani na Dar Indian Ocean, huku
kiingilio kikitarajiwa kuwa Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh 30,000 viti
maalumu.
Wadhamini wa shindano hilo
ni Redd’s Original, Kitwe General Traders, CXC Africa, Jambo Leo, Clouds FM,
Michuzi Media Group, Father Kidevu, Glitters Salon, EFM,UhuruMarathon na Habari
Mseto Blog.
No comments:
Post a Comment