HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 11, 2014

MJUMBE WA BUNGE LA KATIBA AJERUHIWA

  Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Samuel Sitta akimjulia hali mjumbe wa Bunge Maalum kutoka kundi la 201, Thomas Mgoli aliyelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kujeruhiwa na watu wasiojulikana, wakati akipata huduma katika duka moja lililopo karibu na mahali anapoishi mjini Dodoma. (Picha na Owen Mwandumbya)
Mh. Edward Lowassa akimjulia hali Mgoli hospitalini.

 DODOMA, Tanzania

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka kundi la 201,Thomas Mgoli amelazwa katika hospital ya mkoa Dodoma baada ya kudai kupigwa na watu wasiojulikana.

Mgoli amesema alishambuliwa na vijana hao usiku majira ya saa moja eneo la Area D anakoishi.

Amedai kuwa hukutana na vijana hao mara kwa mara anapokwenda dukani na huzungumzia masuala ya bunge hilo, lakini walimshambulia kwa kumwambia kuwa yeye ni CCM.

No comments:

Post a Comment

Pages