HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 12, 2014

BENKI YA CRDB YAZINDUA HUDUMA YA INDIA DESK

Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), wakizindua kwa pamoja huduma mpya ya India Desk  inayowaunganisha wawekezaji na wafanyabiashara nchini India kufanya huduma za kibenki bila ya kuwa na akaunti nchini. Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay, mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi, Ally Laay (kushoto), Celina Mkonyi (kulia). Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay, mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi, Ally Laay (kushoto), Celina Mkonyi (kulia).
Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay wakiwa na furaha baada ya kuzindua huduma hiyo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma India Desk inayotolewa na Benki ya CRDB.

Wadau wa Benki ya CRDB.
Wadau mbalimbali wa Benki ya CRDB.
 Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (katikati) akiwa na maofisa wa Benki hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya India Deski.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya India Deski uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi mpya ya India Desk inayotolewa na Benki ya CRDB.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) na  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (kushoto) wakisakata rhumba wakati wa hafla hiyo.



 Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (katikati) akicheza muziki wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya India Deski inayowaunganisha wawekezaji na wafanyabiashara nchini India kufanya huduma za kibenki bila ya kuwa na akaunti nchini. Kushoto ni mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Ally Laay. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.

 Balozi wa India nchini, Shri Debnath Shaw akizungumza wakati wa
wa uzinduzi wa huduma ya India Desk inayotolewa na Benki ya CRDB.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiwaongoza wageni waalikwa kupata chakula.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa huduma ya India Desk inayowaunganisha wawekezaji na wafanyabiashara nchini India kufanya huduma za kibenki bila ya kuwa na akaunti nchini. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.  
DAR ES SALAAM, Tanzania

BENKI ya CRDB, imezindua huduma mpya ya INDIA DESK inayowaunganisha wawekezaji na wafanyabiashara nchini India kufanya huduma za kibenki bila kuwa na akaunti nchini.


Huduma hiyo itawawezesha wafanyabiashara na wawekezaji kutoa fedha katika akaunti walizonazo nchini kwao kupitia CRDB.

Akizungumza jana jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi wa CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema kuwa CRDB itaendelea kuwa karibu na wateja ili kuhakikisha biashara na uwekezaji kati ya India na Tanzania zinafanyika kwa urahisi.

Dk. Kimei alisema kuwa CRDB inajivunia kuwa Benki ya kwanza kuanzisha huduma hiyo ambayo mtu aliyeko India au nchini ataweza kuhamisha fedha zake.  

“Huduma hii itasaidia mtu aliyeko India akitaka kuja kufanya biashara au kuwekeza habebi fedha bali akifika hapa nchini atatumia CRDB kuhamisha fedha zake kutoka katika benki ambazo tumeingia nazo ubia, na vilevile wa hapa nchini ataweza kutumia benki hizo akiwepo kule India”alisema.

Alizitaja Benki walizoingia nazo ubia kuwa ni Benki ya India (BOI) na ICICI ambazo watashirikiana katika kufanya huduma zote za kifedha kati ya Tanzania, India na Burundi huku kila nchi ikitumia fedha yake.

Balozi wa India nchini, Shri Debnath Shaw, alisema kuwa India ni marafiki na Tanzania na uzinduzi wa huduma hiyo itasaidia wafanyabiashara na wawekezaji walioko India kushiriki kikamilifu katika soko la pamoja la huduma za kifedha na uwekezaji.

Hii ni nchi ya pili kwa benki hiyo kuunganisha huduma za kifedha kwa wawekezaji na wafanyabiashara ambapo Juni mwaka jana iliingia ubia na benki za nchi China.

No comments:

Post a Comment

Pages