Mkufunzi wa FIFA Felix Tangawarima akizungumza wakati wa ufunguzi wa
kozi ya waamuzi na makocha ya Copa Coca-Cola iliyofanyika kwenye uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam. (Na Mpiga Picha Wetu)
NA SARAPIA JUSTINE
MKUFUNZI wa waamuzi kutoka Shirikisho la Soka Duniani FIFA, Felix Tangawarima kutoka Zimbabwe amesema jijini
Dar es Salaam kuwa programu ya waamuzi chipukizi wa mpira wa miguu
Tanzania ni mfano wa kuigwa na nchi nyingine barani Afrika.
“Kwa jinsi nilivyoona, programu ya waamuzi chipukizi hapa
Tanzania imepiga hatua kubwa kwa kuwa na vijana wengi wenye uelewa mkubwa
kuhusu masuala ya uamuzi wa mpira wa miguu tofauti za nchi nyingine”, alisema
Tangawarima wakati wa ufunguzi wa kozi ya waamuzi na makocha wa Copa Coca-Cola.
Tangawarima aliungwa mkono na mkufunzi mwingine wa FIFA
Ulric Mathiott kutoka Seychelles ambaye anaendesha kozi hiyo ya siku tano kwa
upande wa makocha. Mashindano ya Copa Coca-Cola yatafanyika mwezi ujao katika
ngazi ya mkoa na Taifa.
Katibu Mkuu wa Shiriksho la Soka Tanzania (TFF) Selestine
Mwesigwa na Mkurugenzi wa Ufundi Salum Madadi wamewataka makocha na waamuzi hao
vijana kufuatilia kwa makini semina hiyo inayoendeshwa kwa nadhalia na vitendo.
“Ni matarajio yetu kwamba mtaitumia semina hii kuboresha viwango vyenu vya
ukocha na uamuzi na hatimaye kuboresha mashindano ya Copa Coca-Cola”, alisema
Mwesigwa.
Kwa upande wake, Meneja Bidhaa wa Coca-Cola Tanzania Maurice
Njowoka amewashukuru wakufunzi wa FIFA kwa kuja kutoa mafunzo na kusisitiza nia
thabiti ya Coca-Cola kuendelea kushirikiana na TFF na wadau wengine wa soka
nchini kuendeleza mchezo huo hapa nchini.
Washiriki wa semina hiyo ni Ahamed Simba kutoka Mwanza, Ali
Kagile (Kagera) Alloyce Mayombo (Pwani), Andrew Zoma (Tabora), Anthon Mwamulima
(Mbeya), Athman Kairo (Morogoro), Bakati Ali (Pemba Kaskazini), Charles Mayaya
(Shinyanga), Fidelis Kalinga (Iringa) na Gabriel Gunda (Singida).
Wengine ni Hafidh Mucha (Pemba Kusini), Hamis Mabo (Kigoma),
John William (Geita), Joseph Asey (Shinyanga), Joseph Haley (Manyara), Jumanne
Mtambi (Kilimanjaro) Lenard Jima (Ruvuma), Madenge Omari (Mara), Mohamed Muya
(Dodoma), Nicholous Kiondo (Ilala) na Nurdin Gogola (Temeke).
Wengine ni Osuri Kosuli (Simiyu), Peter Amas (Arusha),
Ramadhan Ramadhan (Mjini Magharibi), Renatus Mayunga (Kinondoni), Samwel Moja,
(Lindi), Safe Bakari (Katavi), Shaweji Nawanda (Mtwara), Heha Rashid (Unguja
North) Tigana Lukinjo (Njombe), Yusuf Hamis (Unguja Kusini), Zahor Mohamed
(Tanga) and Zacharia Mgambwa (Rukwa).
No comments:
Post a Comment