HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 14, 2014

TAA yaipatia shule ya Yombo madawati 100


Mkurungezi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleman Suleman, (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa madawati kwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo, Abdallah Ally. Kulia ni Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Christina Kasyupa. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurungezi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleman Suleman, (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa madawati Mwalimu Mkuu wa Shule ya  Msingi Yombo, Christina Kasyupa.

Na Mwandishi Wetu


MAMLAKA ya viwanja vya ndege Nchini (TAA) imetoa msaada wa madawati 100 yenye jumla ya thamani ya shilingi milioni kumi kwa shule ya msingi Yombo iliyopo Kata ya Wilayani Jijini Dar es Salaam.


Msaada huo ulikabidhwa jana na  Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Suleiman Saidi Suleiman kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Chiristina Kasuka, na kushuhudiwa na wanafunzi, walimu pamoja na wafanyakazi wa shule hiyo.  


Akizungumza maraa baada ya makabidhiano, Suleiman alisema amefikia maamuzi hayo kutokana na jitihada za shule hiyo katika kufaulisha wanafunzi na kuona ipo haja ya kuwatengenezea mazingira bora walimu ya kufundishia.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi endapo shule itakuwa na mzingira bora ya kujifunzia, ni wazi kwamba wanafunzi wataheshimu elimu watakayoipata ambayo ndio msingi wa mafanikio.


Kuhusu sula la kudhibiti wa utoro miongoni mwa wanafunzi, alisema atawapeleka wahandisi kupima na kufanya kazi ya kujenga uzio akiamini kwamba itawapunguzia walimu kazi ya kuwalinda wanafunzi kutoroka na nguvu zote kuzielekeza katika kuwafundisha na kufanya vizuri zaidi darasani.


Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuitaka kamati ya shule hiyo kusaidiana katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili shule,ili kuendelea kutekeleza kwa vitendo mpango wa Serikali wa matokeo makubwa sasa (BRN) katika sekta ya elimu.



Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Chiristina Kasuka  alisema msaada huo ni uthibitisho wa uzalendo kwa TAA katika kuthamini elimu.


Alisema shule hiyo ambayo imeanza mwaka 1962 ina walimu 12 na wanafunzi 122,madarasa 15 na nyumba moja ya mwalimu na mwaka jana imefanikiwa kufaulisha asilimia 85.


Pia katika mafanikio mengine alisema wameweza kupata cheti daraja A kwa wakaguzi  wa nje na kuitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha inaendeleza mafanikio yaliyopo ili kuwawezesha wananchi kupata elimu eliyo bora.


Kutokana na msaada huo alisema hivi sasa watakuwa wana upungufu wa madawati 50 tu ambako wakiyapata hawatakuwa na shida hiyo tena.

No comments:

Post a Comment

Pages