HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 14, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Jeshi la Ulinzi la Wananchiwa Tanzania (JWTZ), linatarajia kuzindua huduma ya Tiba kwa jamii kuanzia tarehe 15Agosti2014 hadi 19 Agosti2014 kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi 12:00 jioni katika viwanja vya Mnazi mmoja. Huduma hizi zinakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya JWTZ.

Huduma zitakazotolewa ni pamoja na vipimo vya magonjwa ya Homa ya Ini (Hepatitis B& C), Presha, Kisukari, HudumazaUshaurinasahanakupima VVU, Huduma za uchangia damu salama, Macho, Kinywana Koo. Kwa vipimo vya Malaria, matibabu yatatolewa hapo hapo. Huduma zote hizo nibure.

Nafasi hii itatoa mwanga wakuweza kuona ueledi wa madakitari wetu wazalendo ambao ni matunda yenu.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Afya Dk. Selemani Seif Rashidi. JWTZ linawakaribisha wananchi wote.

          Tumelinda, tunalinda, tutalindadaimaTaifaletu Tanzania.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habarina Mahusiano
MakaoMakuuyaJeshi, Upanga
S.L.P 9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
KwaMawasiliano zaidi: 0754 - 270136

No comments:

Post a Comment

Pages