Meneja Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya UAP Insurance,
Raymond Komanga akifafanua jambo wakati wa akitangaza mashindano ya gofu yaliyoandaliwa
na kampuni hiyo yatakayofanyika Oktoba 4 jijini Arusha. Kushoto ni Meneja Mkuu
wa Uendeshaji wa UAP Insurance, Michael Kiruti na Meneja Uandikishaji
Bima, Ally Athuman. (Picha na Francis
Dande)
Na Mwandishi Wetu
Mashindano ya wazi ya gofu
ya Arusha gofu championships yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 4 mwaka
huu katika uwanja wa Gymkhana jijini Arusha.
UAP ambao ni kampuni la huduma ya utoaji Bima, uwekezaji na
utawala, uwekezaji wa vitega uchumi na maendeleo, pamoja na kuwa washauri
katika mambo ya fedha na ulinzi wa mali, ndio waandaaji wa mchuano huu.
Akizungumza na waandishi
wa habari Dar es salaam Meneja Biashara wa Kampuni ya UAP Insurance Tanzania
inayoratibu michuano hiyo Raymond Komanga alisema wanatarajia kushirikisha
wachezaji wa gofu wa rika zote kutoka jijini humo na hata maeneo mengine ya
jirani
Komanga alisema lengo la
michuano hiyo ni pamoja na kuwashukuru wakazi wa jiji la Arusha kutokana na
ushirkiano wao na kampuni hiyo.
Wachezaji watakaojitokeza
kushiriki katika mashindano haya watanufaika kutokana na
kwamba watakuza vipaji vyao, kujenga afya pamoja na kukuza wigo wao wa
washiriki wa kibiashara kupitia mchezo wa gofu, hivyo tunaomba wachezaji gofu
wajitokeze siku hiyo.
Kwa sasa UAP inafanya kazi katika nchi 6 Afrikazikiwemo
Kenya, Uganda, South Sudan, Rwanda, DRC na Tanzania. Baadhi ya
bidhaa na huduma za UAP ni pamoja na Bima ya mazao , Bima Mifugo , Bima ya
magari, Bima ya mabasi na lori , Bima ya Ndani, bima ya matibabu, bima shule ,
dhima ya umma , bima ya ajali ya makundi au binafsi , bima yamoto na hatarizingine
na mengine zaidi.
Komanga alisema lengo
lingine ni kutaka kuona michuano hiyo inapata washiriki wengi ili kutoa
ushindani na kwamba huo ni mwanzo kwani bado watandaa michuano mingine.
Tutahakikisha tunaandaa michezo mbalimbali
ikiwemo huu wa gofu na ipo lingine
la kuandaa jijini Arusha ni kuhakikisha inakuwa na wachezji wengi wazuri mchezo huo ambao baadaye wataweza kuichezea
timu ya taifa na klabu mbalimbali8 alisema.
Alisema mshindi wa kwanza
katika michuano hiyo atapata zawadi ya kulipiwa bima ya nyumba anayoishi pamoja
na watu wawili anaoishi nao pili atalipiwa bima ya gofu kwa mwaka mmoja wakati
mshindi wa tatu atalipiwa bima ya ajali ya aina yoyote ndani ya mwaka.
No comments:
Post a Comment