TAASISI ya Kuzuia, Kupambana
na Rushwa (Takukuru), imesema katika kumuenzi Mwalimu Nyerere dhidi ya rushwa,
Watanzania wanatakiwa kutoa ushirikiano katika kuwataja baadhi ya watu
wanaojihusisha na vitendo hivyo baadala ya kulalamika tu.
Mkuu wa Elimu ya Raia kwa
Umma wa Takukuru, Stella Mpanju, aliyasema hayo juzi, wakati wa Kipindi cha
Malumbano ya Hoja kinachorushwa na kituo cha luninga cha ITV, akibainisha
kwamba mapambano dhidi ya rushwa ni ya Watanzania wote.
Alisema, itakuwa ni makosa
kwa baadhi ya watu kufikiria kuwa Takukuru itafanikiwa katika mapambano hayo
bila ya ushirikiano wa wananchi ambao anaamini wanawajua wala rushwa katika
maeneo yao.
“Mnawajua wanaojihusisha na
vitendo vya vya ulaji rushwa kwani miongoni mwenu mnawajua sasa bila kuwataja
itakuwa ni vigumu kwa watu hao kuchukuliwa hatua, haiwezekani Takukuru
ikajikamatia watu bila ya kuwa na ushahidi, haya ni masuala yakisheria,
watajeni halafu mtuachi hiyo kazi sisi,”alisema Stella.
Aliongeza kwa wataka kuacha
kulalamika na kuitupia lawama Takukuru huku wakisahau wajibu na uwajibikaji
katika kuzuia vitendo hivyo,ambapo
baadhi yao ndio chachu vitendo
hususan wanapohitaji kupatiwa uhuduma kwenye maeneo mbalimbali yanayotoa
huduma.
“Wote hapa mnalalamikia
vitendo hivyo, lakini huwa najiuliza mla rushwa ni nani, hata nyie hapa
nikiwauliza nani anakula rushwa wote hapa hamtakuwa na jibu, ni lazima
tukaelewa kuwa vita hii inahitaji ushirikiano na jamii ibadili mitazamo dhidi
ya mapambano haya.
Awali
mmoja wa shiriki aliyejitaja kwa jina moja la Likwepa aliwataka Takukuru kuacha
kukukwepa majikumu yao, kuwaachia wananchi kazi yao ambayo inawafanya wapate
mishahara.
“Jamii
inapokosa maadili inaogopa kupambana na watu wanaokula rushwa, pia rushwa
imekuwa sana baada ya kuanzishwa Azimio la Zanzibar ambalo lilivunja mihimili
yote ya Azimio la Arusha,”alisema Likwepa.
Gervas
Lutaguzinda, mshiriki katika mjadala huo, alisemakosa kubwa walilofanya
watawala wa sasa ni kuua Azimio la Arusha ambalo lilikuwa na miiko ya uongozi,
iliyoongoza mapambano dhidi ya rushwa.
“Mfano
mwl Nyerere aliwtaka viongozi wa serikali wasijihusishe na biashara, lakini
baada ya kuvunjwa azimio la Arusha siasa za nchi hii zinaendeshwa na
wafanyabiashara ambao wamekuwa wakitumia rushwa kununua ubunge, udiwani na vyeo. vingine,”alisema.
No comments:
Post a Comment