Ng’ombe hao ambao wamenunuliwa kwa mkopo
uliotolewa na Covenant Bank wana uwezo wa kuzalisha maziwa zaidi ya Lita 20 kwa
siku. Akizungumza na wakazi wa eneo hilo Waziri Kamani ametanabaisha kuwa mikopo ya aina hiyo italeta mapinduzi
makubwa katika sekta ya mifugo.
“Kitendo cha kukabidhiwa Ng’ombe kwa kikundi cha
wafugaji wadogo wa Somangira kinafanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya
nchi yetu hususan katika sekta ya mifugo, Mikopo ya aina hii imekuwa ikitolewa i
kwa Ranchi za taifa lakini haikuwahi kutolewa kwa wafugaji wadogo wadogo” alisema
Dk. Kamani na kuongeza kuwa,.
“Hatua hii ni ya kupongezwa sana hasa kutokana na
Uhitaji mkubwa wa Maziwa uliopo nchini kwa sasa, ambapo kama nchi tunatakiwa
kuzalisha lita bilioni 9 za maziwa kwa siku ili kuwatosheleza watu wetu lakini
kwa sasa tuna uwezo wa kuzalisha lita bilioni mbili tu, Hivyo ninaomba benki
hii kwa kushirikiana na wadau wengine waendelee kutoa mikopo hii kwa vikundi
vingine ili kuongeza uzalishaji”. Alisema.
Aidha, Dr Kamani aliwataka wana kikundi hao
kuhakikisha wanawatumia ng’ombe hao katika kujipatia kipato na kurudisha mikopo
hiyo kwa wakati ili kuwezesha vikundi vingine kukopa kupitia marejesho hayo.
Awali, akizungumza na wananchi wa Somangira Mkurugenzi
wa Covenant Bank, Bibi Sabetha Mwambenja amesema ng’ombe hao 83 wamekatiwa bima
hivyo endapo gg’ombe hao watakufa au kupatwa na tatizo lolote kampuni ya bima itachukua
jukumu la kumlipia mkopo wake mfugaji aliyeathirika.
“Licha ya kutoa mikopo ya ng’ombe kwa hawa wakulima,
Covenant Bank, tumekwenda mbali zaidi kwa kuwawezesha wakulima hawa kupata
mafunzo ya ufugaji wa kisasa wa Ng’ombe wa Maziwa kutoka kwa wataalam wa bodi
ya maziwa na tayari mabanda yamekaguliwa na kujiridhisha kuwa sasa watakuwa
mahali salama’’, Alisema.
Kwa Upande wake Katibu wa Kikundi hicho Bi. Getrude Mpelembe, aliishukuru Benki
hiyo huku akitoa wito kwa Serikali kuboresha miundombinu kwa wafugaji wadogo
kwa kuwapatia wataalam wa kutosha na kutafuta soko la maziwa la uhakika.
No comments:
Post a Comment