Mkurugenzi wa Fedha wa TDL, Bwana
Michael Brown (KUSHOTO) akipokea Ngao ya ushindi kwa TDL baada ya
kuibuka mshindi wa kwanza kama Mlipa Kodi Bora katika kundi la Viwanda,
na Naibu Waziri wa viwanda na Biashara Bw Kigoma malima ndie
anaemkabidhi tuzo hiyo. KONYAGI ilinyakuwa tuzo mbili za ulipaji kodi
bora.
Waziri Kiongozi mstaafu Vuai Nahodha
akimkabidhi Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya TDL watengenezaji wa
KONYAGI bw. Michael Brown Tuzo ya Mshindi wa Jumla ya Mlipa Kodi Bora
katika hafla iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere
Convention centre Wengine katika Picha ni Joseph Chibehe meneja mauzo na Edward Mashingia meneja wa Fedha.
Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya TDL watengenezaji wa KONYAGI bw. Michael Brown akiwa na tuzo aliyoipokea.
Maofisa mbalimbali wa makampuni mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa tuzo za ulipaji kodi bora nchini.
Joseph Chibehe meneja mauzo wa kampuni ya KONYAGI kushoto akibadilishana mawazo na Ofisa wa TBL ambao nao walinyakuwa tuzo.
Baadhi ya washiliki walionyakua tuzo za ulipaji kodo bora wakitoka ukumbini na tuzo zao
No comments:
Post a Comment