Na Bryceson Mathias, Kikombo
MWENYEKITI wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mtaa wa Kikombo Makulu, Eliakimu Kutusha
amesema, Chama chake kitaibuka Mshindi na kuzoa Viti vyote vya Kata ya Kikombo
kwenye Uchaguzi wa SAerikali za Mitaa.
Akizungumza baada ya
kushinda kura ya Maoni ya Chadema Novemba 7, mwaka huu, Kutusha alisema, hakuna
Ubishi Chadema Kata ya Kikomo, kitazoa viti vyote vya Serikali za Mitaa kwa
sababu Chama chake kina wagombea wazuri wanaokubalika na kimejipanga.
Kutusha alipuuza
majigambo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) akisema, “Majigambo hayo ni kama ya
Nyani Mtoto aliyechekelea Msitu unapoungua, huku akiwa hajui utakapoungua usiku
atakuwa hana Nyumba kulala”
Wajumbe wa Chadema walioshinda
katika Kura hiyo ya maoni katika Mtaa wa Makulu na ambao watachuana na wale wa
CCM ni pamoja na, Amosi Matata, Yohana Ndahani, Elia Nyagani, Aidani Mbavu, Roy
Mbalayi, na Pendo Mazengo.
Wananchi waliohojiwa
baada ya kura hiyo ya maoni, wengi wamesema, Kikosi hicho cha Washindi ni
Kikali kwa sababu ndicho kilichowezesha kumng’oa mmoja wa watendaji Kata na
Polisi wa Kata, waliokuwa Mzigo katika Kata hiyo.
Mitaa ya Kata ya
Kikombo ambayo iko kwenye kinyang’anyiro hicho ni Mitatu ambapo, imetajwa kuwa
ni pamoja na Kikombo Makulu, Kikombo Mnandani, ambapo Mgombea wake ni, Ilumbo
Ndaga, na Mtaa wa Kikombo Chololo, ambapo washindi watajulikana kesho.
Naye Mgombea wa Udiwani
wa Kata ya Kikombo Chadema anayetarajiwa kugombea kiti hicho akiridhiwa na
Chama chake, Yona Kusaja, amedai, kama atakuwa na Kikosi kilichopitishwa katika
kura hiyo ya maoni, Ushindi wa Udiwani kwake Kikombo, ni kama Maji ya Kunywa.
No comments:
Post a Comment