Redd's Miss Tanzania 2014 aliyevua taji lake, Sitti Mtemvu.
Na Mwandishi Wetu
REDD’S Miss Tanzania Sitti
Abbas Mtemvu ameamua kuvua taji la Redds Miss Tanzania
alilovikwa usiku wa Oktoba 11 mwaka huu katika Ukumbi wa Mliamani
City, jijini Dar es Salaam.
Katika barua yake ya Novemba 5, kwenda kwa Kamati ya Miss Tanzania, Sitti alisema ni kutokana na shutuma
dhidi yake tangu alipotangazwa mshindi wa shindano hilo.
“Mimi Sitti Abbas Mtemvu,
baada ya kutwaa taji la urembo la Miss Tanzania mwaka 2014 kumezuka shutuma
mbalimbali dhidi yangu, ameniwekea maneno
mengi sana mdomoni kwamba
nimesema wakati siyo.
“Shutuma hizo zimeandikwa katika
vyombo mbalimbali vya habari, Blogs na Mitandao ya Kijamii, kiasi ambacho naona
inaweza hata kuhatarisha maisha yangu.
“Sasa kwa hiari yangu mwenyewe, tena bila kushawishiwa
na mtu na kwa kulinda
heshima yangu pamoja na familia
yangu, natamka rasmi kuvua taji la urembo la Miss Tanzania 2014.
“Napenda niwashukuru
wale wote waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo nilipoingia katika
mashindano haya katika ngazi ya Taifa,
nao ni warembo wote wa Chang’ombe, Temeke, pamoja na wote tuliokuwa nao katika fainali za Taifa.
“Pia napenda kutuma shukrani za dhati kwa waandaaji wote
wa kituo cha Chang’ombe, Temeke na Wajumbe
wa Kamati ya Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali niliyoyapata.
“Nawashukuru pia waandishi wa
habari wote kwa mchango wenu , pamoja na
Wizara ya Habari , Utamaduni na Michezo na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa
busara zenu.
“Leo nalivua rasmi taji
nililopewa na binadamu, lakini taji alilonipa Mwenyezi Mungu, bado
ninalo, mwisho naomba radhi wote kwa uamuzi huu niliouchukua.
Naye Lundenga akizungumzia
uamuzi huo katika hotel ya JB Belmont alisema wamepokea barua hiyo Novemba 6 na
hawana budi kuuheshimu.
Binti huyo amefikia uamuzi
huo mgumu kutokana na kuandamwa kwa madai ya
kudanganya umri kati ya uliopo katika nyaraka mbalimbali ikiwemo pasi ya
kusafiria, leseni ya udereva na ule wa shindano hilo.
“Tumepokea barua ya Sitti, hivyo nafasi yake itachukuliwa na
aliyekuwa shindi wa pili (Lilian Makazima) ambaye ni Miss Arusha na Miss Kanda
ya Kaskazini,” alisema Lundenga.
Kuhusu zawadi zenye jumla ya
sh. Mil 18, alisema hivi sasa ni mapema mno kujibu suala hilo hivyo taratibu za kiofisi zitafuatwa na
watatoa tamko.
Kamazima alisema anafurahia
kupata nafasi hiyo ya kuwa Miss Tanzania hivyo ataanza kwa kujipanga na kufanya kazi
za kijamii ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake ya kuiwakilisha nchi Miss World
hapo mwakani.
Lundenga aibu hii iwe fundisho kwako binafsi pamoja na taasisi yako. Upendeleo ulianza siku nyingi leo umekuwa dhahiri. Uamuzi ufuate haki tu.
ReplyDeleteLundenga, upendeleo ufike mwisho. Aibu hii utaiweka wapi sura yako? Upendeleo ulianza zamani na sasa Mungu ameamua kukuaibisha ili ujifunze.
ReplyDelete