HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 19, 2014

MAALIM SEF AWATAKA MADEREVA KUFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

 Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akimjuilia hali mzee Shihab Ahmed ambaye ni miongoni mwa majeruhi wa ajali ya gari iliyotokea eneo la Kitope, mkoa wa Kaskazini Unguja walipokuwa wakielekea kwenye mkutano wa hadhara wa CUF. Kati kati ni daktari Abdulaziz Mohammed wa  hospitali ya Mnazimmoja mjini Zanzibar. (Picha na Salmin  Said, OMKR)

Na Mauwa Mohamed Mussa, Zanzibar
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewataka madereva kufuata sheria za barabarani kikamilifu ili kuepuisha  ajali ambazo matokeo yake ni kusababisha maisha ya watu kupotea na wengine kupata ulemavu

Alisema hayo wakati akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kuangalia majeruhi wa ajali ya gari    ambao wamelazwa katika hospitali ya rufaa Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar  ajali  iliyotokea Jumapili iliyopita katika eneo la daraja la Kitope, mkoa wa Kaskazini Unguja.

Aliwataka  maderea wote wakiwemo wale wanaoendesha magari ya mizigo kama vile ya mchanga kuchukua tahadhari kubwa wanapokuwa barabarani ili kuepusha ajali zisitokee.

Maalim seif alisema  amepata faraja kubwa baada ya kuelezwa na madaktari dhamana kuwa majeruhi hao wote wanaendelea vizuri na matibabu na afya zao ni nzuri.

Alisema walipata ajali hiyo walipokuwa wakielekea Fukuchani, Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja kuhudhruia mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho na kuhutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa, Mhe. Juma Duni Haji.

Akitoa maelezo juu ya maendeleo ya afya za majeruhi hao kwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Daktari Abdulaziz Ahmed amesema majeruhi wote afya zao ni nzuri na wanaendelea kupata matibabu bila ya matatizo yoyote.

Majeruhi hao ambao wamelazwa katika hospitali ya Mnazimmoja walipata ajali hiyo walipokuwa wakielekea Fukuchani, Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja kuhudhruia mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho na kuhutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa, Mhe. Juma Duni Haji.

Ajali hiyo iliyotokea katika daraja la Kitope ilitokea baada ya gari aina ya Fuso iliyokuwa limebeba sheheana ya mchanga ilipoigonga gari aina ya Hiace walimokuwemo majeruhi hao pamoja na abiria wengine ambao jumla walikuwa 12. 

No comments:

Post a Comment

Pages