HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 19, 2014

Taswa yawaomboleza Karashani, Munyuku



Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha Waaandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya waandishi wawili wa habari za michezo na burudani nchini, Inocent Munyuku na Baraka Karashani (pichani).

Kwa mujibu wa taarifa ya Taswa kwa vyombo vya habari ya jana mchana, Baraka alifariki dunia jana mchana katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.  

Baraka amewahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari, ikiwemo New Habari (2006) Ltd na Nipashe.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa, kifo kingine ni cha Munyuku aliyefariki dunia usiku wa kuamkia, leo.

Munyuku aliyefikwa na kifo akiwa mfanyakazi wa New Habari Ltd, amewahi kufanya kazi vyombo kadhaa ikiwemo Mwananchi Communications Ltd na Uhuru Publication Ltd.

Kupitia taarifa hiyo iliyosaniwa na Kamtibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando, vifo hivyo ni pigo kwa waandishi wa habari za michezo na wanamichezo kwa ujumla.

“Baraka na Munyuku wameondoka wakati bado mchango wao ukihitajika sana,” ilisema taarifa hiyo.
Mhando alisema, taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kwa njia mbalimbali. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.

1 comment:

Pages