HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 23, 2014

Mamia kushiriki maonensho ya elimu Dar

Na Mwandishi Wetu
ZAIDI ya washiriki 500 na watembeleaji 350,000 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajia kushiriki katika maonesho ya kwanza ya kimataifa ya elimu nchini (TIEE).

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link Ltd, Abdulmalik Mollel (pichani) alisema maonyesho hayo yanaandaliwa na kampuni yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade).

Alisema lengo la maonesho hayo ni kuwatambulisha wadau wa masuala wa elimu ili kutoa huduma kwa wananchi na kuwaelimisha juu ya mambo muhimu yaliyopo katika kila sekta.

“Maonyesho haya yanaleta manufaa makubwa na changamoto chanya hasa katika kuongeza ushindani kwenye sekta ya elimu ambayo itasaidia mpango wa matokeo makubwa sasa,” alisema huku akisisitiza kwamba yanawalenga wanafunzi wa rika na kada zote.
Mkurugenzi Mkuu wa Tan Trade, Jacqueline Maleko alisema ili kufanya vizuri katika mambo mbalimbali yanayohusu biashara ni lazima kuwa na elimu ya kutosha, hivyo maonesho hayo yatawasaidia wanafunzi kupata elimu bora itakayowasaidia kufanyabiashara zao kwa umakini.

Aliwataka wanafunzi na wazazi kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo yatakayoanza Desemba 10 hadi 14 katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages