HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 09, 2014

UJIO MPYA WA MWANAMUZIKI TOXSTAR NA VIDEO IJULIKANAYO KAMA 'OLE'

NA SYLVESTER DAVID
MWANAMUZIKI maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini maarufu kama Toxstar ameachia video ya ngoma yake mpya ijulikanayo kama Ole aliyomshirikisha Spince Seseme.

Akizungumza na HABARI MSETO BLOG alisema video hiyo imebeba radha ambayo anaamini mashabiki wake wataipenda.

Toxstar ambaye awali aliwahi kutamba na ngoma ya Pretty Girl aliyokuwa amemshirikisha Alli Kiba na tukutane kitaani aliyoimba na Bob Junior alisema,audio ya wimbo huo imetengenezwa na producer mkali anayekuja kasi ajulikanaye kama Zest Mkali huku video imefanywa na kampuni mpya ya Gallax Media chini ya director Genious Jeff.

Pia Toxstar aliwataka mashabiki wake kuisapoti video hiyo na kwani anaamini ni video bora na ipo katika kiwango kinachostahili


No comments:

Post a Comment

Pages