HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 26, 2014

Wafanyakazi wa Airtel kuwaunganisha wadau katika kusaidia shule ya msingi Kumbukumbu-Dar

  Wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake maalumu wa “Airtel tunakujali” imeandaa matembezi ya hisani huku ikialika wadau wote wenye wito wa kuchangia elimu kuungamkono jitiada hizo ili kukamilisha lengo la kuikarabati shule ya msingi kumbukumbu iliyopo kinondoni jijini Dar es Saalam.

Matembezi hayo yanayoandaliwa na wafanyakazi wa Airtel yatashirikisha wadau mbalimbali na yatafanyika siku ya Jumamosi tarahe 29/11/2014 kuanzia saa moja asubuhi katika viwanja vya ofisi ya Airtel Makao makuu Morocco.

Akiongea kuhusu Matembezi haya Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema “wafanyakazi wa Airtel nao wameona mapungufu yaliopo shuleni hapo na kuamua kujitosa kwa kutumia sehemu ya kipato chao kuihudumia jamii kwa njia hii, kila mfanyakazi wa airtel ambae amehamasika tayari ameshachangia.

Na sasa tumeona ni vyema kuishirikisha jamii pia wakiwemo wanafamilia, marafiki na wote wenye wito wa kuchangia elimu kuungana nasi kuhakikisha watoto wanaosoma shule ya kumbukumbu wanasoma katika mazingira mazuri

“Lengo ni kukusanya zaidi ya shilingi milioni 10 ili kukarabati darasa moja na kununua madawati kwa ajili ya darasa la wanafunzi wa darasa awali”

Tutafanya Matembezi ya Kilomita 5 ambapo ni ya wazi ili kila mtanzania aweze kushiriki na kuchangia, pia kutakuwa na Tshirt maalumu zinapatikana katika ofisi ya Airtel Makao Makuu kwa gharama ya shilingi 15,000. Kwa kununua lengo ni kumfanya kila mmoja aweze kuchangia.

Tunatoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kuungana nasi katika matembezi haya kwa kununua tshirt hizi maalumu na kwa kujitokeza kutembetea nasi ili kuwezesha vijana wetu ambao ni taifa la kesho kupata elimu bora ,katika mazingira mazuri  na yaliyoboresha zaidi. Aliongeza Hawa


Airtel chini ya mpango wa”Airtel Tunakujali” unaoendeshwa na wafanyakazi katika vitengo mbalimbali umeshika kasi ambapo kitengo cha huduma kwa wateja kilifanya burudani na kumshirikisha banana zoro na mzee king Kikii na sasa kitengo cha rasilimali watu na ofisi ya mkurugenzi imeandaa matembezi ya hisani lengo likiwa ni kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia maeneo mbalimbali yanayozunguka jamii hususani kwenye elimu ambapo utekelezaji wake unategemea kutafanyika mapema mwakani.

No comments:

Post a Comment

Pages