Bibi Harusi Mtarajiwa Noreen Mhina akiwa katika nyuso ya Furaha, jana tarehe 25.11.2014.
Bibi Harusi Mtarajiwa Noreen akiwa amempata Mume wake mtarajiwa Leonard Baada ya kumsaka ukumbi Mzima kwa ajili ya kumtambulisha kwa wageni waalikwa .
Bibi harusi Mtarajiwa Noreen akimvisha Mume wake mtarajiwa Leonard zawadi ya Saa Mara baada ya kutambulishwa Rasmi wa wageni waliofika katika Sherehe ya kumuaga.
Bwana Harusi Mtarajiwa Leonard akionesha zawadi yake ya saa aliyonunuliwa na Mke wake mtarajiwa Noreen ikiwa ni moja ya zawadi ya kufika kwake katika sherehe hiyo.
Mume Mtarajiwa Leonard wa Noreen akiwa anamlisha Chakula Mkewe Mtarajiwa ishara ya Upendo.
Msemaji wa upande wa Bwana harusi mtarajiwa akiwakaribisha Rasmi katika harusi upande wa wazazi wa Noreen, Ndugu jamaa na marafiki na kutoa nasaha chache. Jana Tarehe 25.11.2014.
Meza
ya wazazi wa upande wa Bibi harusi mtarajiwa wakiwa wanasikiliza Nasaha
kutoka kwa msemaji wa upande wa Bwana Harusi mtarajiwa.
Wadada wa Mujini nao walimwagia pesa za kutosha Noreen.
Baadhi ya Marafiki wakubwa wa Noreen aliosoma nao katika chuo cha CBE Dodoma.
Palikuwa hapatoshi hapa ambapo Noreen na Bwana Harusi Mtarajiwa Leonard pamoja na wageni wengine waalikwa walicheza kwaito ya nguvu.
Burudani ya Nguvu inaendelea hapa..
Kama kawaida wale mapaparazi wa kujitegemea hawakosi kupata ukodaki wa nguvu kwa ajili ya Facebook, Twitter, Instagram, Whatsapp na kwengine kwingi kuifanya sherehe kuwa inanoga zaidi
Baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia Sherehe na kufurahi.
Bibi Harusi Mtarajiwa akiwa anapunga mikono kuaga wageni waalikwa ishara ya kuondoka ukumbini kwenda kupumzika na kujiandaa na harusi huku akisindikizwa na wapambe wa kutosha.
No comments:
Post a Comment