HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 01, 2014

Airtel yakabithi kisima cha maji kwa shule ya msingi Kumbukumbu Dar

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akifungulia maji ya bomba kama ishara ya uzinduzi rasmi wa  kisima kipya cha maji safi kilichojengwa  kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na Wafanyakazi wake,  katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, wakati wa hafla iliyofanyika shuleni hapo eneo la Block 41 jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani (wa tatu kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Priscilla Moshi (wa nne kushoto). (Na Mpiga Picha Wetu)

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani, funguo za kisima kipya cha maji safi kilichojengwa  kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na Wafanyakazi wake,  katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, wakati wa hafla iliyofanyika shuleni hapo eneo la Block 41 jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Malya (kushoto), Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Priscilla Moshi (wa tatu kushoto), na Mwenyekiti wa Shule hiyo, Mwemba Mwilima.

No comments:

Post a Comment

Pages