HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 01, 2014

BENKI YA POSTA TANZANIA (TPB) KUWAKOPESHA WANACHAMA WASTAAFU WA NSSF

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango maalum wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa NSSF unaojulikana kwa jina la Wastaafu Loan.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza wakati wa uzinduzi wa mikopo kwa wanachama wastaafu wa NSSF 'Wastaafu Loan'  jijini Dar es Salaam.
Meza Kuu.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
 Wadau wakiwa meza Kuu.
 Baadhi ya maofisa wa Benki ya Posta wakiwa katika hafla hiyo.
 Meza Kuu.
 Picha ya Pamoja.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kulia) akibadilishana mkataba wa mikopo na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Crescentius Magori kwa wanachama wastaafu wa NSSF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Crescentius Magori (kushoto) akibadilishana mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi wa mikopo kwa wanachama wastaafu wa NSSF jijini Dar es Salaam jana.  (Picha na Francis Dande)
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori.
 
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Posta Tanzania (TPB) kwa kushirikiana na Mfuko wa Pensheni wa NSSF wamezindua mpango maalum wa kutoa mikopo kwa wastaafu unaojulikana kama kwa jina la Wastaafu Loan.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Sabasaba Moshingi ,alisema lengo la mkopo huo ni kuwawezesha wastaafu kukidhi mahitaji halisi ya fedha na kuboresha maisha yao.

Alisema kwa muda mrefu taasisi mbalimbali za fedha zimekuwa hazitoi mikopo kwa wastaafu kwa kufikiria kuwa  hawana uwezo wa kulipa na kuwajengea dhana ya kutokopesheka.

“Kwa kuliona hilo na kutambua mchango wa wastaafu kwa taifa hili,TPB kwa kushirkiana na Shirika la taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wamebuni mpango huu wa kipekee nchini wa kuwakopesha wastaafu wa mfuko wa NSSF,alisema.

Moshingi alisema kuwa utafiti uliofanywa umeonesha kuwa wastaafu kwa ujumla wanaingiza kiasi kikubwa cha fedha katika kuleta athari chanya katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuongeza uwezo wa kifedha katika taasisi za kifedha ,kuongeza ajira ,kukuza kipato kama fedha hizo wakizitumia vizuri.

Mkurugenzi uendeshaji wa Mfuko wa NSSF Crescentius  Magori alisema mkopo huo ni wa kwanza na wa aina yake  katika soko la mabenki hapa nchini na kwamba utampa amani mwanachama wa NSSF ambaye amestaafu.

“Nina amini kwamba mkopo huu utamfanya mstaafu kuendelea na maisha ya kawaida bila kuwa na hofu au wasi wasi kuhusu changamoto mbalimbali atakazo kutana  nazo katika maisha ya kila siku,”alisema Magori.

Pia aliongeza kuwa mikopo hiyo imeanza kutolewa rasmi jana (leo) katika matawi yote ya benki ya TPB na kwamba mstaafu atakayetaka kukopa hatahitajika kuwa na dhamana ,na kwamba una bima .

Alifafanua pia kwa mstaafu anayetaka kukopa anatakiwa kwenda tawi lolote la benki hiyo lililopo karibu kwa ajili ya kupata huduma za haraka na bora.

“Na sasa wataweza  kunufaika na huduma za kimtandao kwa kuendelea  kupokea pensheni zao kupitia benki yetu,na kwa kufanya hivyo watssfu hawatalazimika kwenda benki kupanga foleni ili wapate fedha zao,”alisema Magori.

No comments:

Post a Comment

Pages