HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 15, 2014

Kinondoni yajivunia kipaji cha Diamond


 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kushoto) akipokea kombe la ushindi wa kwanza katika kukimbiza mbio za mwenge kitaifa 2014, kutoka kwa Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam, Edmund Otieno baada ya manispaa hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kulia) akimkabidhi Meya wa Manispaa ya Kinondoni kombe la ushindi wa mbio za mwenge kitaifa 2014, baada ya manispaa hiyo kuibuka washindi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni akiwa amebeba kombe la ushindi wa kukimbiza mbio za mwenge kitaifa 2014. Sherehe hizo zilikwenda sambamba na kutambua michango ya wadau mbalimbali waliowezesha manispaa hiyo kuwa mshindi wa kwanza kitaifa katika ukimbizaji mwenge.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni akizungumza katika hafla hiyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana akizungumza katika hafla hiyo.
 Kikundi cha Uhamasishaji Manispaa ya Kinondoni wakicheza muziki wakati wa hafla hiyo.
 Watumishi wa Manispaa ya Kinondoni pamoja na wageni wengine wakifuatilia sherehe hizo.
Wakuu wa Idara.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana akikabidhi cheti.

Na Mwandishi Wetu

UONGOZI wa Manispaa ya Kinondoni, umesema unajivunia mafanikio ya kimuziki ya ndani na nje ya nchi ya msanii Naseeb Abdull ‘Diamond,’ kwamba ni fahari ya aina yake kwao kutokana na kuwa mmoja wa wakazi wa wilaya hiyo.

Kupitia umahiri huo wa Diamond katika muziki wa kizazi kipya, wilaya hiyo inajivunia kwani sio tu amekuwa akiitangaza kitaifa, pia amekuwa akiibeba Tanzania kwa ujumla kimataifa. 

Kwamba, mbali ya kujivunia mafanikio ya msanii huyo, pia Manispaa hiyo itahakikisha sekta nyingine ikiwemo ya michezo na utamaduni, inafanya vizuri katika kuendelea kuiletea sifa wialaya hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Musa Natty, katika sherehe ya kutambua michango ya wadau mbalimbali waliowezesha manispaa yake kuwa mshindi wa kwanza kitaifa katika ukimbizaji mwenge kitaifa.

Mhandisi Natty alisema Diamond licha ya kuwa na mafanikio makubwa kwa sasa pia amekuwa na mchango katika manispaa ya Kinondoni kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa watoto wa wilaya hiyo kuendeleza vipaji vyao.

“Tunaye Diamond Platnumz katika manispaa ya Kinondoni huyu ni mtoto wa Tandale na mafanikio yake yanazidi kutufanya wana Kinondoni tutembee vifua mbele na sisi tunatambua mchango wake”alisema Natty.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa hiyo Yusuph Mwenda alisema mbali na Diamond wilaya yake imeweza ku miliki timu ya daraja la kwanza yenye jina la utani Kinoboy, ambayo mpaka sasa inafanya vizuri katika michezo yake.
 
Pia Mwenda alisema katika kuendeleza michezo shule za wilaya ya Kinondoni zimeshiriki michezo ya shmussemita na kuwa washindi wa tatu kitaifa.

No comments:

Post a Comment

Pages