HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 15, 2014

Coastal Union kukipiga na Mwadui FC ya Shinyanga

NA MWANDISHI WETU,TANGA

 MABINGWA wa soka Tanzania Bara mwaka 1988 Coastal Union “Wagosi wa
Kaya”inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Mwadui ya
Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote kujiandaa na
michuano wanayokabiliana nayo.

Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Jumatano ya wiki hii kwenye uwanja wa
CCM Mkwakwani lengo likiwa ni kukipa makali kikosi cha Coastal Union
kujiwida na mechi yao ya Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Tanzania
Prison itakayochezwa kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Akizungumza leo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema
kuwa mechi hiyo ni miongoni mwa michezo mbalimbali ya kirafiki
wanayocheza ili kuweza kukiimarisha kikosi hicho ambacho msimu huu
kimepania kufanya makubwa kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania.

Assenga amesema kuwa timu ya Mwadau ya Shinyanga inatazamiwa kuwasili
mkoani hapa Jumanne wiki hii tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao
unatazamiwa kuwa na upinzani mkali.

Hata hiyo aliwataka wadau wa soka mkoani hapa kujitokeza kwa wingi
kushuhudia mchezo huo ikiwemo kuangalia wachezaji ambao wamesajiliwa
msimu huu kwa ajili ya michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.

Hata hivyo alisema kuwa baada ya kumalizika mechi hiyo wataangalia
uwezekano wa kucheza mechi nyengine ya kirafiki kabla ya kutua jijini
Mbeya ambapo watakwenda kucheza mechi yao ya Ligi kuu.

No comments:

Post a Comment

Pages