Rais Jakaya Kikwete akimtunuku Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Nne, Stephen Hiza (Mgosingwa) kwa niaba ya Atomic Band.
Na Mwandishi Wetu
BENDI ya Muziki wa Dansi Atomic Jazz imeingia katika vitabu vya historia
ya nchi baada ya kutunikiwa nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya muungano
daraja la nne.
Nishani hiyo ilikuwa ni moja ya nishani mbalimbali zilizotolewa kwa
watunukiwa na Rais Jakaya Kikwete, wakati wa maadhimisho ya sherehe za maadhimisho ya miaka
53 ya uhuru wa Tanganyika, zilizofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Rais Kikwete, aliitunuku Atomic Jazz Band nishani hiyo kutokana na kazi
yao kubwa katika kulihamasisha taifa kuenzi muungano.
Miongoni mwa nymboa ambazo zimekuwa kichocheo cha kudumisha amani na
umoja ni ule unasema ,Tanzania nchi yangu yenye furaha’ ambao umekuwa ukichezwa
kwenye redio mbalimbali.
Kwa nishani hiyo Atomic Jazz Band inakuwa ni bendi ya kwanza ya muziki
wa dansi kupata nishani katika kipindi cha miaka 50 ya muungano.
Akizungumzia nishani hiyo, Stephen Hiza (Mgosingwa), ambaye ni mmoja wa wanamuziki wa bendi hiyo,
alisema ni jambo la kujivunia kwani inaonesha ni jinzi gani Rais Kikwete alivyotambua
kazi za bendi hiyo katika kipindi chake.
Bendi hiyo ilianzishwa mwaka 1954, miongoni mwa wanamuziki waliowahi
kuwemo katika bendi hiyo ni mwenyewe Hiza, Mbaraka Mwinshe, Michael Vicent na
wengine.
No comments:
Post a Comment