HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 11, 2014

UTT-AMIS YATOA WITO KWA WATANZANIA KUJITOKEZA KATIKA MASUALA YA UWEKEZAJI

 Ofisa Mafunzo na Masoko wa UTT-AMIS, Waziri Ramadhani akitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliofika katika banda lao wakati wa Maonyesho ya Maadhimisho ya Miaka 53 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kuzishirikisha Taasisi zake kwa lengo la kuangalia mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka 10 ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Kulia ni Ofisa Uendeshajiu wa UTT-AMIS, Justine Joseph.
  Ofisa Mafunzo na Masoko wa UTT-AMIS, Waziri Ramadhani akitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliofika katika banda lao wakati wa Maonyesho ya Maadhimisho ya Miaka 53 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kuzishirikisha Taasisi zake kwa lengo la kuangalia mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka 4. Kulia ni Ofisa Uendeshajiu wa UTT-AMIS, Justine Joseph na kushoto ni Ofisa Masoko, Pauline Kasilati.
 Baadhi ya watu waliohudhuria maonyesho hayo wakisikiliza hotuba kutoka kwa mgeni rasmi wakati wa kufungwa kwa maonyesho hayo.
Maofisa wa UTT-AMIS wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maonyesho hayo kutoka kushoto ni Ofisa Masoko wa UTT-AMIS, Pauline Kasilati, Ofisa Uendeshaji,  Justine Joseph na Ofisa Masoko, Waziri Ramadhani.
 
Na Mwandishi Wetu

WATANZANIA wametakiwa kujitokeza katika masuala ya uwekezaji kwani fursa hiyo wanayo kama ilivyo kwa baadhi ya watu kutoka nje.
Hayo yalisemwa na Ofisa Habari Idara ya Masoko, Waziri Ramadhani, wakati wa maonesho ya kuadhimisha miaka 53 ya Uhuru wa Tanganyika, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Alisema hivyo kutokana na baadhi ya watu hapa nchini kudhani kuwa ili mtu awe muwekezaji ni lazima atoke nje ya nchi wakati sio kweli.
“Nawaomba Watanzania wenzangu watambue kuwa wao pia ni sehemu ya wawekezaji hivyo basi wasijitenge wanaposikia fursa kama hizi na baadala yake wajitokeze, waje wawekeze katika mfuko huu wa UTT,” alisema Ramadhani.
Alisema mfuko huo baada ya kuyabaini hayo umeamua kufikisha elimu katika jamii kwa kutumia njia mbalimbali, ambayo anaamini itawajengea uwezo wa uwelewa kuhusu jinsi ya kuwekeza.
Ramadhan, alisema Mfuko wa Umoja ulianzishwa mwaka 2005, ni mfuko unaolenga kutimiza mahitaji tofauti ya wawekezaji huku ukitoa faida.
Alizitaja baadhi ya faida hizo kuwa ni uwekezajiulio wazi kwa kila mtanzania; vipande vinauzwa kwa bei ya soko (hakuna ada ya kujiunga).
Nyingine ni mwekezaji anaweza kununua vipande kumi, kuna urahisi wa kujiunga na kujitoa wakati wowote pindi mwekezaji anapotaka kufanya hivyo.
Hata hivyo ofisa huyo, alitoa rai kwa Watanzania kuwa ili kujua mengi zaidi kuhusu mfuko huo wanaweza kufika katika ofisi zao kila mahali zilipo.

No comments:

Post a Comment

Pages