Kamati ya
Mpira wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imetupa rufani ya timu ya Mwanza kupinga uhalali wa wachezaji wawili wa Kigoma
kwenye mechi yao ya robo fainali iliyochezwa jana (Januari 26 mwaka huu) Uwanja
wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mwanza
iliyopoteza mechi hiyo kwa mabao 2-1 iliwalalamikia wachezaji Neema Sanga na
Vene Dickson wa Kigoma kuwa waliwahi kuchezea timu ya Taifa (Twiga Stars),
hivyo kucheza mashindano ya Kombe la Taifa la Wanawake ni kinyume cha kanuni.
Kamati
baada ya kupitia rufani hiyo, imeitupa kwa vile timu ya Mwanza haikuwasilisha
vielelezo vyovyote kuthibitisha madai hayo dhidi ya wachezaji hao. Pia Kamati
yenyewe ilipitia taarifa za Twiga Stars ambapo haikupata kumbukumbu za
wachezaji hao katika timu hiyo.
Pia
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya TFF imesikitishwa na kitendo cha
viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) Mkoa wa Mwanza
kugomea uamuzi dhidi ya rufani yao, hivyo imependekeza Mwenyekiti wa TWFA
Mwanza, Sophia Tigalyoma na Katibu wake Hawa Bajanguo wapelekwe Kamati ya
Nidhamu kwa hatua za kinidhamu.
WASHINDI COPA COCA-COLA WAKABIDHIWA VITITA VYAO
Washindi
wa Copa Coca-Cola 2014 wamekabidhiwa zawadi zao za fedha kutoka kwa mdhamini wa
michuano hiyo ya umri chini ya miaka 15 kwa wavulana na wasichana kampuni ya
Coca-Cola. Fedha hizo kwa washindi mbalimbali tayari zimeingizwa kwenye akaunti
zao.
Kwa
upande wa wavulana; washindi na kiwango walichopata ni mabingwa Dodoma (sh.
milioni nane), makamu bingwa Kinondoni (sh. milioni tano), mshindi wa tatu
Kigoma (sh. milioni tatu) wakati timu yenye nidhamu Tanga (sh. milioni moja).
Mchezaji
bora Mwami Ismail kutoka Kigoma (sh. 500,000), mfungaji bora Timoth Timoth wa
Dodoma (sh. 500,000), kipa bora Kelvin Deogratia wa Geita (sh. 500,000) na
mwamuzi bora Abdallah Mbarome kutoka Zanzibar sh. 500,000).
Kwa
upande wa wasichana ni mabingwa Kinondoni (sh. milioni tano), makamu bingwa
Ilala (sh. milioni tatu), mshindi wa watatu Temeke (sh. milioni mbili) wakati
timu yenye nidhamu Mbeya imepata sh. milioni moja).
Zubeda
Mohamed wa Kinondoni ambaye ndiye mchezaji bora amepata sh. 500,000, mfungaji
bora Stumai Abdallah wa Temeke sh. 500,000 wakati kipa bora ni Suleta Saad wa
Zanzibar sh. 500,000.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment