HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 15, 2015

NSSF-REAL MADRID SPORTS ACADEMY WAANZA USAJILI WA VIJANA WATAKAOJIUNGA NA KITUO KIPYA CHA MICHEZO

Msajili wa Vijana katika Program ya NSSF - Real Madrid Sports Academy, Haji Ramadhani (kushoto) kutoka Idara ya Michezo na Elimu ya Viungo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akimwandikisha, Revocatus Raphael (kulia) huku baba yake mzazi, Raphael Evarist akishuhudia.

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII (NSSF) kwa  kushirikiana na  klabu ya Real Madrid  ya Hispania, limezindua rasmi mchakato wa usajili wa  vijana walio na umri wa chini ya miaka 14 watakaofanyiwa majaribio kwa ajili ya kujiunga na kituo cha michezo cha NSSF-REAL MADRID SPORTS ACADEMY
Mchakato huo wa usajili umeanza leo kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam ambako  watoto kutoka manispaa za Temeke Ilala, na Kinondoni wameanza kuandikishwa. Zoezi hilo linatarajia kuendelea kesho Tarehe 15/02/2015 na mwishoni mwa wiki ijayo tarehe 21 na 22 februari 2015. 

Vijana walengwa katika zoezi hilo ni wale waliozaliwa kuanzia Januari , 2001 hadi Disemba, 2002. 

Katika zoezi hilo Mtoto anatakiwa kuambatana na mzazi wake au Mlezi anayetambulika kisheria na aje na uthibitisho wake kuwa ni mlezi halali kwa kuonyesha vithibitisho vya kisheria.

Kwa mtoto husika,  aje na Cheti halisi cha kuzaliwa na kopi yake pamoja na picha za paspoti zenye rangi ya bluu. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika uwanja wa Karume Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF Ndugu Crescentius Magori alisema jukumu la NSSF ni kuratibu usajili wa vijana  wengi iwezekanavyo  ambao watafanyiwa majaribio ambapo vijana 500 watakoonyesha uwezo watakabidhiwa kwa wataalamu kutoka Clabu ya Real Madrid ili   kufanyiwa majaribio zaidi na mwishowe kupata wachezaji 30 ambao wataingia rasmi katika awamu ya kwanza kabisa katika kituo hicho cha michezo kinachosubiriwa kwa hamu hapa Nchini.

Ndugu Magori ametoa wito kwa wakazi wote wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kuwaleta watoto wao ili wapate fursa hii muhimu kwao.

No comments:

Post a Comment

Pages