1.
UTANGULIZI
Katika
wiki ya pili ya Februari 2015, baadhi ya watoa huduma za mawasiliano ya simu za
mkononi walianzisha vifurushi vya mawasiliano na bei na kusabababisha
malalamiko kutoka kwa watumiaji na umma kwa ujumla. TCRA, kwa kuzingatia upeo
wa shughuli zake, imechambua hali hiyo na inapenda kutoa maelezo na maagizo
ambayo yatawezesha kuondoa sintofahamu iliyopo na kujenga mustakabali kwa siku
zijazo.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania ya mwaka 2003, miongoni mwa
kazi za TCRA ni kufuatilia utoaji wa huduma katika sekta inazozisimamia
kwa kuzingatia kiwango cha upatikanaji wa huduma hizo, ubora na viwango vya
huduma, bei ya huduma na kuhimiza ushindani
na ufanisi wa kiuchumi. Katika kutelekeza majukumu yake, TCRA
inawajibika kupitia na kuchambua, mara kwa mara, utoaji wa huduma katika sekta
na kuchukua hatua dhidi ya chochote kinachotokea kwenye soko, kiwe chanya au
hasi.
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania inaongozwa na Sera za Kisekta, Sheria ya Mamlaka ya Mawasilioano Tanzania ya 2003,
Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta
(EPOCA) ya 2010, na Kanuni zake za mwaka 2011 zilizotungwa kwa
kuzingatia matakwa ya EPOCA. Kifungu 6(1) cha Sheria ya TCRA kinaitaka Mamlala
kufuatilia utoaji wa huduma unaofanywa na sekta inazozisimamia ikiwa ni pamoja
na upatikanaji, ubora na viwango vya huduma, gharama za huduma hizo na
kufanikisha ufumbuzi na utatuaji wa malalamiko na migogoro. Hivi karibuni kumekuwa
na malalamiko kuhusu tozo mpya zilizotangazwa na makampuni ya simu za mkononi.
2.
UKUAJI
WA SEKTA YA TEHAMA
Kumekukuwepo
na kukua na kubadilika kwa haraka kwa soko la mawasiliano Tanzania katika
kipindi cha miaka 10 iliyopita. Mwaka 2005, kwa kuzingatia mabadiliko ya TEHAMA
duniani kote, Tanzania ilianzisha mfumo wa leseni unaozingatia muingiliano wa tekinolojia.
Mfumo huo unajulikana kama “converged licencing framework”; kwa kifupi, CLF
ambamo, aina nne za leseni zilianzishwa. Hizo ni leseni inayomwezesha mwekezaji
kujenga miundombinu na kutoa huduma; leseni inayowezesha kutoa huduma ama kwa
kutumia miundombinu anayomilki mtoa huduma au anayokodisha; leseni ya kuwezesha
utoaji wa huduma kama vile za mawasiliano ya intaneti, huduma za kifedha
kupitia mtandao na leseni kwa ajili ya maudhui ya utangazaji wa televisheni na
redio.
Soko
la TEHAMA limekuwa kwa idadi ya watumiaji wa huduma hizo, kwa aina mbalimbali
za huduma hizo na kwa kuongezeka kwa eneo ambamo huduma mbalimbali zinapatikana;
ingawaje idadi ya watumiaji wa simu za mezani imepungua. Kuna laini za simu za
mkononi zipatazo 31,862,656 sasa ukilinganisha na laini 2,963,737 mwaka 2005;
kama iliyoonyeshwa hapo chini. Idadi ya simu za mezani ni 151, ukilinganisha na
154, 420 mwaka 2005. Watumiaji wa
intaneti wameongezake hadi kufikia 11,000,000 Desemba 2014 kutoka 3,563,732 mwaka
2008. Kwa sasa, kuna hamu kubwa ya matumizi ya intaneti na mwelekeo huu
utaendelea; hasa kutakapokuwa na ongezeko la mitandao inayowezesha kutoa huduma
za intaneti; na kuongezeka kwa mitandao ya jamii.
3.
AINA
NA MPANGILIO WA TOZO
Watumiaji
wa TEHAMA wanapata aina kuu tatu za huduma, ambazo ni:
·
Huduma
za sauti (kuzungumza)
·
Huduma
ya ujumbe mfupi wa meseji, kwa kifupi SMS (Short Message System)
·
Intaneti
Wateja
walionunua laini au ambao wanatumia huduma za simu kwa kuzungumza imeongezeka
kwa asilimia 91 kutoka milioni tatu (3,000,000) mwaka 2005 hadi milioni 32 ( 32,000,000) mwaka 2014. Hii
imewezesha huduma za simu kufikia asilimia
97 ya Watanzania ilipofika Desemba 2014; kutoka asimilia 10 mwaka 2005. Kwa
upande mwingine, muda wa kuzungumza kwa simu, ukiwa umepimwa kwa dakika
zinazotumika, umeongezeka sambamba na ongezeko la idadi ya watumiaji. Umefikia
dakika bilioni 41 kutioka dakika milioni 506 mwaka 2005.
Matumizi
kwa upande wa meseji, yaani SMS na data pia yameongezeka kwa kiasi kikubwa
kutoka SMS zipatazo milioni 5 mwaka 2005 hadi SMS bilioni 10 mwaka 2014.
Watumiaji wa intaneti wanaotumia simu za mkononi sasa wanafikia milioni 10.
Huduma
hizi zinatozwa na watoa huduma kwa aina mbili za tozo: Kuna tozo za msingi na
tozo mtumiaji anapojiunga na vifurushi. Gharama za kupiga simu zinatozwa kwa
shilingi kutokana na dakika mtumiaji atakazotumia kuongea, gharama za kutuma
SMS zinatozwa kwa kila ujumbe mfupi unaotumwa na zile za intaneti na data zinatozwa
kwa ‘uniti’ ambazo mtu anatumia. Uniti hizi zinaitwa ‘bytes’, kwa mfano, “Megabytes”
au kwa kifupi MB na Gigabytes ambazo ni MBs 1,024. Hivyo, matumizi ya intaneti yanatozwa kwa MB
au GB mtu anazotumia. Hivi karibuni
watoa huduma wametangaza vifurushi vipya ambavyo vimesababisha malamiko kutoka
kwa baadhi ya watumiaji.
3.1
TOZO ZA MSINGI
Katika
kipindi cha miaka miwili iliyopita kumekuwa na kupungua kwa ujumla kwa tozo za
msingi kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali linalofuata, baada ya kuzingatia
ongezeko la jumla la bei (inflation). Ni vyema ikazingatiwa kwamba gharama za
muingiliano kati ya watoa huduma; yaani kiasi ambacho watoa huduma wanalipana
kwa kuwezesha watumiaji wa mitandao mingine kutumia mitandao yao kimekuwa
kikipungua. Taarifa hiiinachambua tozo
za vifurushi. Iwapo mtumiaji hatajiunga na kifurushi, tozo za msingi
zinatumika.
3.2
AINA NA MPANGILIO WA VIFURUSHI
Watoa
huduma za simu kwa kawaida wanatoa mpangilio wa tozo kwa wateja wao sambamba na
tozo za msingi. Vifurushi ni mpangilio ambao mtumiaji anachagua yeye mwenyewe
kwa kupenda. Hata hivyo mpangilio huu umetokea kupendwa sana na weatumiaji. Kwa
kawaida vifurushi vinauzwa kwa huduma za
mazungumzo, za kutuma meseji na za intaneti.
Mtumiaji anaweza
kujisajili kutumia kifurushi ama cha siku, wiki au mwezi. Tutachambua
mipangilio hii katika majedwali yanayofuata.
3.2.1
VIFURUSHI VYA
MAZUNGUMZO, MESEJI NA INTANETI
3.2.1.1 VIFURUSHI
VYA SIKU VYA MAZUNGUMZO, MESEJI NA INTANETI
Jedwali 1: Idadi ya Dakika, Meseji kwa bei za
chini na za juu kwa Siku
|
|||||||||
|
|
Baada
|
|||||||
Bei (TZS)
|
Dakika
|
SMS
|
MB
|
Bei
|
Dakika
|
SMS
|
MB
|
||
Vodacom
|
399
|
4
|
50
|
15
|
499
|
7
|
300
|
8
|
|
|
999
|
21
|
1,000
|
100
|
999
|
20
|
1,000
|
8
|
|
Airtel
|
399
|
5
|
50
|
15
|
499
|
9
|
300
|
10
|
|
|
995
|
40
|
Bila Kikomo
|
250
|
999
|
24
|
1,000
|
10
|
|
Tigo
|
499
|
7
|
300
|
30
|
649
|
13
|
450
|
8
|
|
|
999
|
21
|
1000
|
100
|
999
|
20
|
1,000
|
8
|
|
Uchambuzi
1:
·
Kuna mabadiliko ya bei na idadi ya dakika na
idadi ya meseji. Hata hivyo mabadiko haya sio makubwa.
·
Kuna upungufu mkubwa wa kiasi cha uniti za
data, MBs.
3.2.1.2 VIFURUSHI
VYA WIKI VYA MAZUNGUMZO, MESEJI NA INTANETI
Tozo, idadi ya
dakika, meseji kwa bei za chini na za juu kwa vifurushi vya Wiki
|
Jedwali 2: Idadi ya dakika, meseji kwa bei
za chini na za juu kwa vifurushi vya
Wiki
|
|||||||||
|
|
Baada
|
|||||||
Bei (TZS)
|
Dakika
|
SMS
|
MB
|
Bei
|
Dakika
|
SMS
|
MB
|
||
Vodacom
|
1,999
|
30
|
500
|
100
|
1,999
|
29
|
500
|
60
|
|
|
4,999
|
90
|
1,000
|
300
|
9,999
|
190
|
1000
|
60
|
|
Airtel
|
1,995
|
60
|
700
|
175
|
1,999
|
34
|
1,000
|
70
|
|
|
5,999
|
200
|
Bila kikomo
|
2,000
|
9,999
|
200
|
5,000
|
70
|
|
Tigo
|
1,999
|
40
|
700
|
300
|
4,999
|
91
|
2,000
|
60
|
|
|
9,999
|
250
|
5,000
|
1,024
|
9,999
|
190
|
5,000
|
60
|
Uchambuzi
2:
·
Kuna mabadiliko ya bei na idadi ya dakika na
idadi ya meseji. Hata hivyo mabadiko haya sio makubwa.
·
Kuna upungufu mkubwa wa kiasi cha uniti za
data,MBs.
3.2.1.3 VIFURUSHI VYA MWEZI VYA MAZUNGUMZO,
MESEJI NA INTANETI
Tozo, idadi ya dakika, meseji kwa bei za chini na za juu kwa vifurushi
vya Mwezi
Jedwali 3: Idadi ya
dakika, meseji kwa bei za chini na za juu kwa vifurushi vya Wiki
|
||||||||||
|
|
Baada
|
||||||||
Bei (TZS)
|
Dakika
|
SMS
|
MB
|
Bei
|
Dakika
|
|
SMS
|
MB
|
||
Vodacom
|
10,999
|
130
|
500
|
300
|
14,999
|
230
|
|
1200
|
250
|
|
|
29,999
|
550
|
2,500
|
800
|
49,999
|
1,000
|
|
3,000
|
250
|
|
Airtel
|
9999
|
175
|
5000
|
400
|
9,999
|
175
|
|
5,000
|
300
|
|
|
49,999
|
1,100
|
10,000
|
2048
|
49,999
|
1,100
|
|
10,000
|
300
|
|
Tigo
|
9999
|
200
|
8,000
|
1,024
|
19,999
|
370
|
|
8,000
|
250
|
|
|
49999
|
1,200
|
10,000
|
4,096
|
49,999
|
1,000
|
|
10,000
|
250
|
Uchambuzi
3:
·
Kuna mabadiliko ya bei na idadi ya dakika na
idadi ya meseji. Hata hivyo mabadiko haya sio makubwa.
·
Kuna upungufu mkubwa wa kiasi cha uniti za
data,MBs.
3.2.2
VIFURUSHI
VYA INTANETI PEKEE.
Kwa ajili ya
kulinganisha,vifurushi vya intaneti tu ndivyo vilivyochambuliwa kwa kuwa ndiyo
huduma ambayo inatolewa na watoa huduma wenye leseni za kutoa huduma za intaneti.
Jedwali 4. Vifurushi
vya Intaneti vya mwezi:
|
|||
|
Bei (TZS)
|
MBs
|
Bei
|
Vodacom
|
2,500
|
100
|
25
|
|
25,000
|
Bila kikomo
|
-
|
Airtel
|
12,500
|
3,000
|
4
|
|
30,000
|
20,000
|
2
|
Tigo
|
15,000
|
1,000
|
15
|
|
25,000
|
Bila kikomo
|
-
|
Zantel
|
6,000
|
600
|
10
|
|
300,000
|
Bila kikomo
|
-
|
TTCL
|
28,000
|
Bila kikomo
|
|
Smile
|
10,500
|
500
|
21
|
|
1,450,000
|
200 GB
|
7
|
Mpangilio
huo wa tozo kwa matumizi ya intaneti kwa mwezi unaonyesha kwamba mtumiaji analipa
kidogo anapotumia uniti nyingi zaidi.Kwa hiyo, mpangilio huu unawafaa zaidi
wale wenye matumizi makubwa ya intaneti.
4.
HITIMISHO,
MAPENDEKEZO NA MAAGIZO:
Kama
tulivyoeleza awali kuna aina mbili za toto: Tozo za msingi na tozo za
vifurushi. Malalamiko ya hivi karibuni ya watumiaji yameelekezwa kwenye
mpangilio na tozo za vifurushi. TCRA imechambua mpangilio wa vifurushi – tozo
za zamani na mpya na kugundua kwamba ingawaje baadhi ya watoa huduma
wamabadilisha bei, kwa ujumba bei za muda wa kuzungumza na idadi ya meseji
hazikubadilika sana. Hata hivyo, kuna upungufu mkubwa kwa idadi ya uniti za
data (MBs).
Kwa
hivyo, TCRA inaagiza kama ifuatavyo:
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania itachukua hatua stahiki za usimamizi kuhakikisha kwamba
watoa huduma wanazingatia matakwa ya sheria. Kifungu cha 5 cha Kanuni za tozo
(EPOCA Tariff Regulations) za mwaka 2011 kinayataka makampuni ya simu
kuwasilisha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania gharama mpya wanazokusudia kutoza
wateja wao kabla hazijaanza kutumika. Mamlaka itatoa adhabu kila inavyobidi.
·
TCRA inaagiza
watoa huduma kuzingatia sheria kila wanapobadilisha bei za bidhaa zao;
(a) Kuziwasilisha
kwa Mamlaka kabla hazijaanza kutumika,
(b) Kutoa
taarifa za tozo za msingi na vifurushi kwa njia ambayo itaweza kuwafikia watumiaji
wa simu za mkonini,
(c) Kupitia upya bei na tozo mpya kwa kuzingatia
mapendekezo haya na kuwasilisha kwa Mamlaka kama inavyotakiwa kwa mujibu wa
Kanuni za EPOCA za 2011 kuhusu tozo ( EPOCA (Tariff Regulation of 2011).
·
TCRA inawaagiza
watoa huduma kuhakikisha kwamba mabadiliko yoyote yanatekelezwa kidogo kidogo
na sio ya ghafla ili kuepuka sintofahamu katika soko;
(a)TCRA inawaagiza watoa huduma kuwapa wateja
wao nafasi ya kuchagua mpangilio wa vifurushi tofauti kwa huduma wanazohitaji:
Kifurushi
cha mazungumzo, Meseji na Intaneti cha
siku, siku saba au mwezi ambacho kinampa
mtumiaji uhuru wa kuchagua kiasi ambacho wako tarari kulipia kwa mazungumzo,
meseji na intaneti.
(b)
Vifurushi
vya mazungumzo tu: Hivi navyo kwa siku, siku saba au siku 30 kwa
ajili ya watumiaji ambao hawahitaji intaneti na meseji kwa sababu moja au
nyingine na wako tayari kulipia vifurushi vya sauti pekee;
(c) Vifurushi cha Meseji (SMS) tu: Kwa watumiaji ambao
hawahitaji intaneti au muda wa mazungumzo kwa sababu moja au nyingine, au ambao
wanatumia SMS kwa wingi. Hivi nayo viwe kwa siku, siku saba au siku 30 kwa bei
ambazo mtumiaji atachagua.
(d)
Vifurushi
vya Intaneti tu: Kwa watumiaji ambao wanatumia intaneti kwa
wingi. Hawa wapewe uhuru wa kuchagua vifurushi vya siku, siku saba au siku 30.
·
TCRA inawashauri watumiaji wa huduma za
mawasiliano kuchagua vifurushi na mpangilio wa tozo ambao unafaa kwa matumizi
yao. Watumiaji wanatakiwa kudai taarifa kamili kuhusu huduma wanazozilipia na
waelewe taarifa za watoa huduma kuhusu bei na tozo, ikiwa ni pamoja na vigezo
na masharti ya huduma.
Mtumiaji asiporidhishwa na huduma anayopata anatakiwa
alalamike – kwanza kwa mtoa huduma wake, na asiporidhika na ufumbuzi awasilishe
malalamiko yake TCRA.
·
Watumiaji wanashauriwa kuchukua fursa ya
soko huria la mawasiliano nchini kama nafasi ya kulinganisha huduma na bei za
watoa huduma na vifurushi wanavyouza kabla ya kuamua kujiunga na kifurushi
chochote au huduma yoyote.
·
Watumiaji wa simu janja zinazowezesha
matumizi ya huduma nyingi, maarufu kama “smart phone”, kuwa makini wakati wa
kuzitumia. Wahakikishe kwamba wanazima maeneo ambayo yanaweza kutumia data hata
kama wakati huo hawatumii vifurushi vya data walivyonunua kwenye vifurushi.
Kwa
taarifa zaidi, wasiliana na TCRA, Na. 20 Barabara ya Sam Nujoma, Dar Es Salaam.
SL.P 474 Dar Es Salaam 14414. Barua
pepe: dg@tcra.go.tz
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
23 Februari
2015
No comments:
Post a Comment