Na Mwandishi Wetu
KITUO
Cha Uwekezaji nchini (TIC) kimesema kinamiliki viwanja viwili na shamba moja
nchini hivyo kama
kuna Kiwanja chenye hati ya TIC basi wao
hawahusiki.
Hayo yamekuja siku chache baada ya waandishi wa
habari kutaka kupata ufafanuzi wa kiwanja chenye namba
40118 kilichopo eneo la Wazo Hill Katika
Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Waandishi wa habari mwanzoni mwa
wiki hii kuhusu hati hiyo Ofisa Mipango Miji wa TIC
Elibarik Wilfred alisema kutokana na hati hiyo
kwa jinsi ilivyo kisheria wao ndio wamiliki halali wa eneo hilo
lakini si kweli kuwa wao ndio wamiliki wa
Kiwanja hicho hivyo hawahusiki nacho.
"Sisi hatumiliki hiki Kiwanja kwani TIC
tunamiliki Viwanja viwili ambavyo ni hiki hapa Dar es Salaam ambapo zipo ofisi
zetu na cha pili kipo Kimandoro Arusha lakini kingine si Kiwanja bali ni Shamba
lililopo Mkulazi Kilombero mkoani Morogoro"alisema Wilfred.
Akizungumzia kuhusu kutumika kwa jina la TIC
kumiliki Kiwanja hicho au Viwanja vingine bila wao kuhusika
wala kutambua alisema hilo ni jambo
lingine.
Kiwanja hicho ambacho kinadaiwa kuwa ndio
ambacho Mafundi Gereji wa Manispaa ya Kinondoni ndipo walipo
baada ya kupelekwa hapo na Manispaa hiyo baada
ya kubomoa gereji zote bubu zilizoko katika Manispaa hiyo ili kuiweka katika
hali ya usafi
Akizungumzia kuhusu hilo Diwani wa Kata ya Wazo
John Murro alisema tayari pia nyaraka hizo zimemfikia
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda.
"Ni kweli Meya naye amezipata na amemwagiza
ofisa wa Mipango Miji na Ofisa ardhi ili kujiridhisha
kuhusu TIC kumiliki Kiwanja
hicho."alisema Morro
Baadhi ya watu waliotoa maoni yao kuhusu sakata
hilo walisema inawezekana jina la TIC lilikuwa
linatumika ili watu wajipatie kula na familia
zao huku wanyonge wakidhulumiwa
Walisema kumekuwa na tabia ya watu wenye fedha
kutumia fedha zao kudhulumu haki za watu wengine sasa
kama TIC wamekana kumiliki Kiwanja hicho basi
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi waweke wazi nani ambaye analipia
Kiwanja hicho ili akamatwe
"Kama kweli TIc
wamekana kumiliki Kiwanja hicho basi wanaokilipia wakamatwe ili iwe fundisho
kwa wengine wenye kudhulumu haki za wenzao ili kujinufaisha wao na familia
zao"walisema watu hao.
No comments:
Post a Comment