Baraza Kuu la
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa
Lindi chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Amir M. Mkalipa, wamefanya kikao
cha kikanuni leo tarehe 21 feb 2018, katika ukumbi wa mikutano wa
ofisi kuu ya CCM Mkoa wa Lindi, iliyopo Wailes, Lindi mjini.
Pamoja na kujadili
hoja zingine zinazohusu uimara wa jumuiya mkoani Lindi, changamoto za
Vijana na Walimu, suala la migomo ya wafanyabiashara, na kuwataka
watendaji wa Serikali kutimiza wajibu na majukumu yao kikamilifu ili
kuongeza ufanisi wa Serikali katika kutatua kero za wananchi na
kuleta maendeleo ya jamii, lakini pia kikao hicho kimeazimia:-
a} Baraza kuu la
UVCCM Mkoa wa Lindi imeitaka Serikali kuendelea kuchukua hatua kali
kwa watakaobainika kuhusika na mauaji ya Albino. Ni lazima Serikali
kushirikiana na wananchi wahakikishe ndugu zetu Albino wanaishi
maisha yenye usalama, amani na furaha kwani ni haki yao kikatiba.
b}Pia, Baraza Kuu la
UVCCM Mkoa wa Lindi linampongeza Mhe. Rais na Mwenyekiti wa CCM ndugu
Jakaya Kikwete kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM (2010-2015) kwa
kukamilisha ujenzi wa barabara ya Kibiti-Mingoyo,
Pia inampongeza Mhe
Rais Jakaya Kikwete kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Lakini pia, UVCCM
inampongeza na kumuunga mkono Mhe Rais kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya
wapya 27 ambapo baadhi ya wateule hao wanatoka kwenye jumuiya hiyo,
jambo ambalo ni heshima kubwa kwa UVCCM, na kudhihirisha kuwa jumuiya
hiyo inatimiza wajibu wake wa kuwa tanuru la kuoka viongozi wenye
uwezo, waadilifu na wenye kuaminika katika jamii. Pia UVCCM
imewapongeza ndugu Mboni Mhita na ndugu Paul Makonda kwa kuteuliwa
kuwa wakuu wa wilaya na kuwataka wakatimize wajibu kwa kuwatumikia
wananchi kwa uadilifu na ufanisi.
Pia, UVCCM Lindi
inampongeza Kamanda wa Vijana Mkoa Mhe Bernard Membe-Mbunge wa Mtama
na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa kwa kuwa karibu
na Vijana na kuiwezesha jumuiya kutimiza majukumu yake.
C} Mwisho, UVCCM
Mkoa wa Lindi inahimiza Halmashauri za wilaya kutenga asilimia 10% ya
Mapato yake kwa ajili ya maendeleo ya Vijana na Wanawake, ili vijana
wanufaike kwa mikopo na waweze kujiajiri ili kukabiliana na tatizo la
ajira na umasikini. Jambo hili lipo kisheria sio ombi, hivyo
watendaji husika wa Serikali wahakikishe wanatimiza wajibu wao
ipasavyo ama UVCCM itawalazimisha kutimiza wajibu huo.
Jumuiya ya Umoja wa
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi, wamepitisha ratiba ya
shughuli zao kwa Mwaka 2015 na wataanza ziara ya kutembelea Vijana
katika wilaya zote sita (6) za Mkoa wa Lindi.
No comments:
Post a Comment