HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 13, 2015

CHAMA KIPYA CHA SIASA CHAZALIWA

 Mwenyikiti wa Chama cha C.K.U.T, Ramadhan Semtawa. Jijini Dar es Salaam akifafanua jambo. Kushoto ni Katibu wa chama hicho, Noel Antapa.
Msajili wa vyama vya  Siasa Jaji Francis Mutungi, (kulia) akimkabidhi hati ya Usajili wa Muda wa chama cha Kijamaa na Uzalendo (C.K.U.T), Mwenyikiti wa chama hicho Ramadhan Semtawa. Jijini Dar es Salaam. 

 Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha siasa ili kiweze kuendeshwa vizuri kwa misingi ya utawala bora na baadae kifikie malengo yake ya kuchukua dola ni lazima kiwe na katiba yenye misingi ya kidemokrasia.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam na Msajili Msaidizi wa Vyama vya siasa, Sisty Nyahoza wakati wa kukabidhi cheti cha muda kwa Chama cha Kijamaa na Uzalendo Tanzania (C.K.U.T).

Alisema demokrasia ya kweli ni muhimu kuanza kujengwa ndani ya chama kwani itawasaidia viongozi  kufikia malengo waliyojiwekea.

Nyahoza alisema viongozi pia wanawajibu wa kusoma sheria ya vyama vya sisasa ili kuepuka migongano na watendaji wa taasisi zingine za serikali.

“Leo tumetoa cheti cha usajili wa muda kwa chama cha C.K.U.T, tunawaomba sana viongozi wa chama hiki kukaa pamoja na wanachama wenu ili kupeana mawazo mazuri ya kujenga chama,asitokee mmoja wapo na kusema kuwa yeye ndiye mwenye chama, hivyo someni vizuri sheria ya vyama ili msiwe na mgogoro na taasisi zingine,” alisema.

Naye Msajili wa Vyama vya Siasa, Mstaafu Jaji Francis Mutungi alisema ofisi ya msajili ni taasisi hivyo itawahudumia watu wote wanaohitaji huduma.

Mwenyekiti wa chama cha C.K.U.T Ramadhani Semtawa alisema wameanzisha chama kwa malengo maalumu ya kurejesha nchi kwenye misingi ya waasisi.

Alisema kumekuwepo kwa rushwa na masuala la kidini  kumechangia nchi kuyumba na kutoka katika misingi ya kidemokrasia na utawala bora.

“Watu wanauwa kwa sababu za kidini na wengine upoteza maisha yao kwa imani za kishirikina, lakini pia wapo watu wamekuwa wakila fedha za serikali na awachukuliwi hatua yoyote, tunataka kuja kuibadilisha nchi hii maana aina muelekea kwa sasa,” alisema.

Semtawa alisema kinachofanyika sasa ni kutafuta wanachama ili waweze kupata usajili wa kudumu.

“Tunatakiwa tuwe na wanachama 2000 katika mikoa kumi na kila mkoa mmoja inatubidi tupate wanachama 200, tumejipanda vizuri na tunaamini kuwa tutapata usajili wa kudumu,”alisema.

Aidha Semtawa alisema awatahitaji kiongozi yoyote kutoka katika vyama vya upinzani kujiunga na chama hicho.

No comments:

Post a Comment

Pages