Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali
Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai maara
alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja
kubhudhuria katika Hitma ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid
Amani Karume Iliyofanyika leo asubuhi. (Picha na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed
Shein (katikati) akiwaongoza Viongozi mbali mbali pamoja na Wananchi katika
Kisomo cha hitma ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid
Amani Karume katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja
Iliyofanyika leo asubuhi.
Baadhi ya Viongozo wakisoma hitma akiwemo aliyekuwa Rais wa Kwanza
wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume(kushoto) Balozi Ali Karume katika
ukumbi
wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui.
wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui.
Waislamu na wananchi mbali mbali wakiwa katika kisomo cha hitma ya aliyekuwa
Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika ukumbi wa
Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandu.
Akinamama wa Mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja wakiwa katika kisomo cha
Hitma ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume
katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui.
Mke wa Rais Zanzibar Mama Mwanamwema Shein(katikati) akiwa na
Mama Shadya Karume Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar(wa tatu kulia) Mama Fatma
Karume (wa pili kulia) Mke wa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mama Zakia
Bilali (kushoto) Bi Khadija Aboud (wa pili kushoto)Mjumbe wa Kamati Kuu wa
CCM,katika hitma ya kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee
Abeid Amani Karume.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali
Mohamed Shein akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza
wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua
iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandu.
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed
Gharib Bilali akiweka
shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid
Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa
Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo.
Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Hamid Ameir akiweka shada la mauwa
katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani
Karume.
Balozi Ali Karume (Mtoto) kwa niaba ya familia akiweka shada la
mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani
Karume.
Wake wa Viongozi wakiitikia dua iliyoombwa katika kaburi la Marehemu
MzeeAbeid Amani Karume baada ya hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya
CCM Kisiwandui Mjini Unguja na kuhudhuriwa na waislamu mbali mbali kutoka mjni na Vijijini.
Wake wa Viongozi wakiitikia dua iliyoombwa katika kaburi la Marehemu
MzeeAbeid Amani Karume.
Baba Askofu wa Anglikan wa Kanisa la Mkunazini Michael Hafidh akiomba
dua wakati Viongozi mbali mbali waliofika katika kaburi la aliyekua Rais wa
Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma
iliyosomwa leo.
No comments:
Post a Comment