Na Bryceson Mathias, Dodoma
WAUMINI wengi wa madhehebu ya Kikristo waliohojiwa kwa
nyakati tofauti mkoani Dodoma wameunga mkono hatua ya maaskofu kumjibu Rais
Jakaya Kikwete kutokana na kusema tamko la Jukwaa la Wakristo (TCF) kuwataka
waumini wao kupigia kura ya ‘hapana’ Katiba Inayopendekezwa lilikuwa la hasira.
Waumini hao wamewaunga mkono maaskofu kufuatia viongozi hao
kujitokeza tena na kusisitiza kwamba msimamo wao utabaki kama ulivyo, ikiwa ni
siku tano baada ya Rais Kikwete akiwa
ameongea na watu wengine si wao.
Katika tamko la pamoja walilolitoa mwanzoni mwa wiki hii
mkoani Dodoma baada ya kukutana,
viongozi hao wamemtahadharisha Rais Kikwete kuwa kuendelea kupigia debe Katiba
Inayopendekezwa na kuruhusu Mahakama ya Kadhi, kunaweza kulitumbukiza taifa
katika machafuko na hali ikiwa hivyo s
Tamko hilo limesainiwa na viongozi walewale waliosaini lile
la awali Machi 12, mwaka huu yaani Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania
(CCT), Askofu Dk. Alex Malasusa, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki
Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na Mwenyekiti wa Kanisa la
Pentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Daniel Awet.
Tamko hilo lenye maneno 921, limeendelea kuwataka waumini
wao kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,
kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kujitokeza kuikataa kwa kupiga kura ya
‘hapana,’.
Msimamo huo wa maaskofu, tayari umeibua msuguano baina yao
na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp
Kardinali Pengo aliyesema viongozi wa dini hawana mamlaka ya kuwaamulia waumini
wao aina ya kura wanayostahili kupiga.
Kwa upande wa waumini waliohojiwa wamedai, hata wao
hawamuelewi pengo anaposema, viongozi wa dini hawana mamlaka ya kuwaamulia
waumini wao aina ya kura wanayostahili kupiga, hivyo wanahoji, mbona viongozi
wa serikali akiwemo rais na mawaziri, wanawaamulia waumini wa kiroho wapige kura
ya ‘Ndiyo?’
Wengine wamekwenda mbali wakisema, historia ya kanisa kamwe
haisemi hata siku moja kama serikali iliwahi kuliongoza kanisa, isipokuwa kanisa
ndilo lililokuwa linaiongoza serikali, hivyo mkanganyiko huo ndio usipofikiwa
maridhiano lazima uigharimu serikali.“Ni vigumu watawala waingie kusema vitu
kanisani, misikitini, halafu wenye makanisa na misikiti wasiseme kitu kwenye serikali,
wakae kimya kama vinyago, hilo halikuwa jambo la busara na hekima mbele za
Mungu na watu,” alisema Benjamin
Kambangwa wa Kanisa Katoliki.
Naye Josephina James wa Kanisa la Anglikana alisema,
viongozi wakuu wa serikali – Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Rais Kikwete
wasifurahie wakidhani ujumbe wao walioongea na viongozi wa Kikristo
wasiostahili umewafikia viongozi wa dini waliozungumza nao hivi karibuni, kwa
kuwa watu waliokutana nao si wawakilishi rasmi na hawana uwezo wa kutoa uamuzi
au kukubaliana juu ya jambo hilo la kitaifa.
Joachim Jackson wa Evangelistic Assemblies of God alisema rais
kuzungumza na wazee wa Dar es Salaam na mkuu wa mkoa na kutafsiri kuwa viongozi
wa dini wana hasira wakati hawaongozwi na hasira wala mihemko katika kufikia
maamuzi, ni kutowatendea haki, maana wao wanaongozwa na maombi na sala, hivyo
wanatakiwa waombwe radhi.
Jumamosi iliyopita, Rais Kikwete akifungua mkutano wa
Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam iliyoshirikisha wajumbe kutoka mikoa
mbalimbali ikijumuisha viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo, alisema
msimamo wa TCF kuhusu kuipigia kura ya ‘Hapana’ Katiba Inayopendekezwa ni wa
hasira na usiokuwa na tija kwa maendeleo ya taifa.
“Nimeyasoma matamko hayo yote kwa umakini, imenishangaza,
imenisikitisha na kunihuzunisha. Siamini kwa nini wamefikia huko kwa kuunga au
kutokuunga mkono,” alisema Rais Kikwete.
Kikwete aliongeza: “Waacheni waumini waamue Katiba
wanayoitaka wao... hayo matamko niliyoyasoma yamejaa hasira kwa serikali
kupeleka bungeni muswada wa Mahakama ya Kadhi.”
Maaskofu hao walikuwa Dodoma kufuatilia kwa kina Muswada wa
Marekebisho ya Sheria mbalimbali ya mwaka 2014 unaopendekeza, pamoja na mambo
mengine, marekebisho ya Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu la mwaka 1964
unaotambua Mahakama ya Kadhi.
No comments:
Post a Comment