Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kuundwa kwa kamati ya pamoja ya utekelezaji wa ajenda za tamko la pamoja la maridhiano ni suala la kisiasa lakini ushiriki wa vyama vya Siasa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK) ni sharti la Kisheria na Kikatiba.
Kwa muktadha huo, CCM kimekitaka ACT Wazalendo kuanza kutekeleza wajibu wa kushiriki serikalini wakati mpango wa kuundwa kwa Kamati ya pamoja ukiendelea kufanyika.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis,aliyesema Vyama vilivyokidhi matakwa ya sheria na kutakiwa kushiriki katika SUK ni faradhi.
Mbeto alisema CCM na ACT vina wajibu na shuruti ya kushiriki kwenye serikalini kutokana na mahitaji ya Katiba huku mchakato wa kuundwa kwa Kamati ya pamoja ya maridhiano, ukiendelea.
Aliwataka viongozi wa ACT Wazalendo kutochanganya masuala hayo mawili kwa wakati mmoja, badala yake akawataka watambue kuwa kila suala lina wakati na umuhimu wake.
"Kuundwa kwa Kamati ya Pamoja ya Maridhiano yenye Wajumbe toka CCM na ACT ni suala la kisiasa. Vyama hivyo vikumbuke ndivyo vyenye dhamana na wajibu wa kisheria na kikatiba hivyo hivina hiyari" alisema Mbeto.
Aidha, alisema vyama hivyo vinapokuwa pamoja serikalini ni rahisi kwao kukumbushana kuhusu utekelezaji wa hatua za kiutendaji za kamati ya pamoja, kuliko chama kimoja kimo Serikalini na kingine kimetoroka.
"Sioni kama kuna tatizo. Kama lipo, liko wapi hadi ACT kianze kusuasua. Kila kitu kiko wazi lakini wenzetu wanataka kujenga taharuki kwa wananchi ionekane kuna mjadala mkubwa bila kujali maslahi ya nchi" alieleza
Makubaliano na hatua za utekelezaji wake ni mchakato usiohitaji shinikizo lolote,ndiyo maana hakuna muda mahsusi toka hatua moja hadi nyigine na badala yake kila kitu kimewekwa kwa mpangilio na uwazi zaidi.
"ACT wasipoteze muda bure. Wasiwatie hofu wananchi kana kwamba kuna jambo kubwa mno lisilowezekana. Kila kitu chini ya jua kinawezekana .Ndovu hajawahi kushindwa kubeba mkonga wake" alisisitiza Mwenezi Mbeto.
Katibu huyo alibainisha kuwa pamoja na mbio zote za kisiasa, bado wananchi wanahitaji kupata huduma muhimu na maisha bora yanayotokana na utendaji wa shughuli za kisera za serikali .
"Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi ndiye mwenye dhamana ya kuteua lamati ya pamoja ya utekelezaji wa ajenda za Maridhiano. Tunamtaka Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Othman Masoud Othman aache pupa na wahka. Zanzibar imepitia mengi na yote yamepita kwa salama" alikumbusha Mbeto.
September 06, 2026
Home
Unlabelled
MBETO AWAKUMBUSHA ACT KUHESHIMU TAKWA LA KATIBA, SHERIA
MBETO AWAKUMBUSHA ACT KUHESHIMU TAKWA LA KATIBA, SHERIA
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.




No comments:
Post a Comment