Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya inayotoa punguzo kabambe kwa gharama za kupiga simu ijulikanayo kama ‘Airtel Zone’, katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi na (kulia) ni Meneja Masoko wa Airtel, Ravi Agarwal.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati), Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi (kushoto) na Meneja Masoko wa Airtel, Ravi Agarwal, wakionyesha bango kama ishara ya uzinduzi wa huduma mpya inayotoa punguzo kabambe kwa gharama za kupiga simu ijulikanayo kama ‘Airtel Zone’, katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
· Kufurahia punguzo la hadi asilimia 99 za kupiga simu ndani ya nchi
· Pungunzo kwa wateja wa Airtel Nchi nzima
xxxxxxxxxxxxxxxxxx
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora na zenye ubunifu nchini leo imeendelea kudhihirisha hilo kwa kuzindua huduma mpya inayotoa punguzo kabambe kwa gharama za kupiga simu (Dynamic Tariffing) Itakayojulikamana kama “Airtel Zone”. Sasa wateja wa Airtel wa malipo ya awali sasa watafaidi kupiga simu kwa gharama ndogo yenye punguzo la hadi asilimia 99 kwa simu za nchini.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora na zenye ubunifu nchini leo imeendelea kudhihirisha hilo kwa kuzindua huduma mpya inayotoa punguzo kabambe kwa gharama za kupiga simu (Dynamic Tariffing) Itakayojulikamana kama “Airtel Zone”. Sasa wateja wa Airtel wa malipo ya awali sasa watafaidi kupiga simu kwa gharama ndogo yenye punguzo la hadi asilimia 99 kwa simu za nchini.
Huduma hii ya Airtel Zone imezinduliwa kwa mara ya kwanza na Airtel ili kuendeleza dhamira yake ya kutoa huduma nafuu za mawasiliano ya simu za mkononi na kutoa fursa kwa wateja wake kuongea zaidi kwa gharama nafuu mara tu watakapo jiunga kwa kupiga namba 107 na kufuata maelekezo au kupiga *149*39# kisha kuchagua ‘0’.
Akiongea wakati wa uzinduzi Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Bwana Levi Nyakundi alisema” uzinduzi wa punguzo la gharama za kupiga simu ni uthibitisho wa dhamira ya kampuni ya Airtel kuwapatia watanzania dili lenye thamani halisia ya fedha zao na kuwawezesha watu wengi zaidi nchini kuwasiliana kirahisi. Lengo letu ni kuendelea kutoa huduma za kibunifu na zenye gharama nafuu ili kukithi mahitaji ya watanzania wote. Wateja wetu watakaojiunga na huduma ya “Airtel Zone” kuanzia leo, sasa hivi wataweza kupiga simu na kupata punguzo la hadi asilimia 99 na punguzo hili litategemea mahali alipo mteja”
“Hii ni punguzo litakalosaidia sana wateja wa Airtel kupata unafuu wa kuwasiliana kibiashara, masomo au kwa kuwasiliana na ndugu jamaa au wapendwa wao bila kuwa na wasiwasi juu ya gharama zao za simu” alieleza bw, Nyakundi
Tunaamini huduma hii ya “Airtel Zone” imekuja kwa wakati muafaka wakati mawasiliano ya simu za mkononi ni nyenzo muhimu katika ukuzaji wa shughuli za kiuchumi na za kijamii aliongeza Nyakundi
Akifafanua zaidi kuhusu huduma hii Mkurugenzi wa Mawasilaiano Bi Beatrice Singano Mallya, alisema” punguzo la gharama litategemea mahali mteja alipo na muda anaopiga simu, mteja atapata ujumbe utakaomuonyesha kiwango cha punguzo anachopata kwa mahali alipo, alikadhalika mteja anaweza kupiga *149*39*0# ili kuangalia kiwango cha gharama ya kupiga simu. Huduma hii ya “Airtel Zone” ni kwa wateja wa malipo ya awali na punguzo hili litatumika kupiga simu za ndani tu .
Sambamba na hilo mteja atakayekuwa na kifurushi cha muda wa maongezi kama vile Airtel yatosha na vifurushi vingine punguzo litaanza pale tu kifurushi chake cha muda wa maongezi kitakapoisha.
Kuujiunga ni rahisi, bure na mara moja tu, piga 107 ufate maelekezo au piga *149*39#” aliongeza, Singano Mallya
No comments:
Post a Comment