Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha akitoa taarifa ya mkutano mkuu wa ishirini wa wanahisa wa Benki ya CRDB unaotarajia kufanyika May 8 jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Mtambuka Benki ya CRDB Bi.Esther Kitoka na kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uendeshaji na Huduma kwa Wateja Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay
Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa akiongea katika mkutano na waandishi wa habari katika maandalizi ya Mkutano Mkuu wa ishirini wa wanahisa wa Benki ya CRDB
Kulia ni Katibu wa Bodi ya CRDB, John Baptist Rugambo, katikati ni Mkurugenzi wa Fedha Frederick Nshekanabo, Kushoto Tully Esther Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja.
Meneja Kitengo cha Huduma kwa Wateja kwa njia ya simu, Ena Mwangama (kulia) na Edwin Nchimbi Ofisa Masoko wakifutilia mkutano huo.
Kulia ni Meneja Usajili wa Hisa kutoka Benki ya CRDB Emmanuel Ng’ui na Dorice Ngikari kutoka ofisi ya Katibu wakifatilia jambo
Mwandishi wa habari kutoka Mwananchi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Arusha Media Mussa Juma akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Crdb Dk. Charles Kimei.
Na Pamela Mollel, Arusha
Kufuatia anguko la shilingi ya Tanzania dhidi ya dola wafanyabiashara nchini wametakiwa kuona kuwa ni fursa ya wao kijiinua kiuchumi katika biashara zao ndani na nje ya nchi na kuachana na propaganda za wanasiasa ambapo wanalalamikia anguko hilo.
Ambapo hali hiyo imesababisha kupanda kwa bidhaa mbalimbali nchini hali inayotajwa kuongeza ugumu wa maisha ya wananchi sambamba na wafanyabiashara nchini ambao wananunua na kuagiza bizaa kutika nje ya nchi.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei wakati akiongea na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mkutano mkuu wa ishirini wa wanahisa wa Benki ya Crdb unatarajia kufanyika kesho jijini Arusha katika kituo cha mikutano cha Kimataifa AICC.
Hata hivyo alisema kuwa hivi sasa Benki hiyo imeweza kupata faida ya shilingi bilioni 95.6 sawa na asilimia 14 kwa mwaka 2014 ambapo limekuwa ni ongezeko kubwa zaidi kutokea ambapo faida hiyo itawasaidia kuweza kupatia wanahisa hao gawio la shilingi 15 kwa kila hisa na idadi ya wanachama hao.
Ambapo mizania imeongezeka kwa asilimia 17 katika lengo lao katika mwaka huu ingawa soko limekuwa gumu kutokana na mfumuko wa bei uliopo sasa.
Dk. Kimei aliongeza kuwa kutakuwepo na ajenda mbalimbali katika mkutano huo mkuu ambapo moja ya ajenda ni kuangalia namna ya kukua zaidi na kuongeza mtaji wao na kuboresha mfumo mzima wa Tehama ili kuweza kukabiliana na wizi wa kupitia mtandao ili kuweza kuwahakikishia usalama wa pesa za wateja wao.
Aidha Banki hiyo inamkakati wa kuongeza mtaji wao ambapo wanatarajia kuongeza zaidi ya billion 100 ili kuongeza aman za banki na mtaji wao ili kuboresha huduma hizo na kukuza rasilimali za banki hiyo.
Dk. Kimei aliongeza kuwa wanamkakati wa kupanua huduma zao katika nchi ya Burundi na nchi jirani ili kuweza kuwarahishishia wateja wao pindi wanapotoka na kutembelea nchi hiyo na kupata huduma ya miamala ya fedha.
Benki hiyo hivi sasa wanamawakala zaidi ya 575 ya fahari huduma na wanamashine ya zaidi ya 375 za kutolea pesa katika mikoa yote nchini ili kuwarahisishia wateja wao kupata huduma za kibenki.
No comments:
Post a Comment