HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 24, 2015

JK AONGOZA KIKAO CHA NEC LEO TENA

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, mjini Dodoma leo, May 24, 2015. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. (Picha na Bashir Nkoromo)
 2. Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akishauriana jambo na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kabla ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kuanza leo.
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, wakiwa kwenye kikao hicho. mstari wa mbele kutoka kushoto ni, Dk. Salim Ahmed Salim, Shamsi Vuai Nahodha na Katibu Mkuu wa CCM, mstaafu, Wilson Mukama.
 Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba na Spika wa Bunge Anna Makinda.
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM,  Bernard Membe na Nazir Kalamagi wakijadiliana jambo kabla ya kikao cha NEC kuanza.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Usi Yahya Haji kutoka Kaskazini Unguja, akimsalimia mjumbe mwenzake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu wakati wakijiandaa kuingia ukumbini kwenye Kikao cha NEC mjini Dodma leo.
 Mjumbe wa NEC, Amina Salum Ali akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT Sophia Simba nje ya ukumbi, kabla ya kikao cha NEC kuanza leo. Kushoto ni Mjumbe wa NEC Asha Abdallah Juma.
 Katibu Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Hamis Sadifa, kabla ya kikao kuanza. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Wajumbe wakiwa ukumbini wakati wa mkutano huo 

No comments:

Post a Comment

Pages