HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 13, 2015

Chadema; Tumejipanga kukabili Njama za Ulaghai wa BVR-Morogoro

 Na Bryceson Mathias, Morogoro

KATIBU wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Morogoro, Samuel Kitwika, amesema, kutokana na uandikishaji wa wapiga kura katika daftari la kudumu kwa mfumo wa ‘Biometric Voters Registration’ (BVR) kupiga Hodi Morogoro, Chadema kimejipanga vizuri kukabili Njama zote za Ulaghai wa BVR Morogoro.

Akizungumza akiwa kituo cha basi muda Mchache kabla ya kuelekea Dodoma kwenye Mkutano wa Watia Nia wa Kanda ya Kati, Morogoro, Dodoma na Singida utakaoanza Juni 14, mwaka huu, Kitwika amewaonya Watendaji wa BVR, Wasithubutu kukengeuke maana wamejipanga kwa hilo.

“Tumejifunza kila Mbinu na Njama chafu za ulaghai zilizotokea Mikoa mingine katika uandishaji, hivyo ninawaonya wasithubutu kufanya ujanja ujanja wowote kwetu, maana tumejipanga kukabiliana na Njama zozote za Uharibifu wa kuzuia watu wasijiandikishe kwa BVR mkoani Morogoro.

“Ninawashauri Wananchi, msisubiri saa mbili asubuhi ya Watendaji hao, ikiwezekana ninyi laleni hapohapo kama ilivyo kwenye Matanga, ili kesho yake asubuhi na Mapema mjiandikishe na hatimae muwahi kwenda mashambani.

“Mbinu zao za Ujanja ujanja wa kwamba, Mashine hazina Mtandao, Hazina Moto, Haziwaki, Nani hajafika, Kuhamisha bila utaratibu au visingizio kuwa Watendaji hawana uzoefu, hatutaki kusikia mkoani Morogoro na Majimbo yake, kwa sababu Changa hili la Macho tunalijua”.alisema Kitwika.

Aliwataka Polisi kuacha, kuepuka tabia ya kuwanyanyasa na kuwatisha Wananchi wakiwa kwenye zoezi hilo kama wanavyofanya kwenye matukio ya Migogoro ya Wafugaji na Wakulima, na badala yake waonesha Uzalendo wa kuwa Walinzi wa watu na Mali zao ili wasitumike Vibaya.

Alisema, kujipanga huko kwa Chadema ni kuhakikisha Uhalali na Haki ya wanaojiandikisha, vinafanyika kwa Amani na Utulivu, kwakutumia Mfumo wa FTP 100, kwa maana ya kwamba kila Jimbo na Kata Mawakala 200.

Aidha amekiri Chadema kupokea Barua ya Ofisi ya Serikali ya Mkoa wa Morogoro, ambayo imetumwa kwa Vyama vyote vya Siasa, ikiwataarifu viongozi wake kwamba, Uandishaji wa BVR mkoani humo, utakuwa kuanzia Juni 16, hadi Julai 16, Mwaka huu, hivyo viongozi wawaandae wananchi.

No comments:

Post a Comment

Pages