NA ELIZABETH JOHN
MSHINDI wa tuzo ya mtumbuizaji bora wa kiume
Afrika (Mtv MAMA 2015), Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameiomba serikali kumpa
sapoti katika kazi nzuri anayoifanya kutokana na kuitangaza vyema Tanzania
katika mataifa mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam, Diamond alisema kuwa, licha ya kuleta tuzo hiyo nyumbani kwa mara
ya kwanza hajaona sapoti yeyote iliyooneshwa na serikali au Baraza la Sanaa la
Taifa (Basata).
Diamond alisema kuwa tuzo aliyoileta nyumbani ni
kubwa hasa ukiangalia hakuna msanii yeyote ambaye alifanikiwa kuipata hivyo
alihitaji sapoti kutoka kwa serikali au Basata kutokana na kazi hiyo nzuri
ambayo imezidi kumjenga Kimataifa.
“Kiukweli nasapotiwa na watanzania ila sio
serikali kwa sababu napata pongezi kutoka kwa kila mmoja kwa nafasi yake,
ingekuwa vizuri kama mkutano huu wa kuwashukuru Watanzania wangeifanya serikali
na sio uongozi wangu hivyo nawashauri Basata wawe wanatusapoti na sisi
tunaofanya vizuri na sio kuangalia nani kakosea,” alisema Diamond.
Nyota huyo aliwashukuru Watanzania kwa kumsapoti
kufanikisha kutwaa tuzo hiyo ambayo anakiri imezidi kumpa fursa ya kutamba
Kimataifa ambapo baada ya kufanya kutumbuiza katika hafla ya utoaji tuzo hizo
zilizofanyika Julai 18 huko Durban, Afrika Kusini mwanamuziki kutoka Marekani
Neyo, aliomba kufanya naye kolabo.
Diamond alisema kwamba changamoto anayokutana
nayo katika muziki wake ni ugumu wa soko la muziki wake, kwamba anapotaka kutoa
kazi lazima aumize kichwa kutambua mashabiki wake wanamsapoti kazi ya aina
gani.
No comments:
Post a Comment