Michuano ya Kombe la Vilabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Kagame Cup) inatarajiwa kuanza kutimua
vumbi siku ya Jumamosi tarehe 18 Julai 2015 jijini Dar es salaam, kwa
kushirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka kwa Nchi
za Afrika Mashariki na kati.
Mashindano ya CECAFA Kagame
Cup ni mashindano makongwe barani Afrika ambayo yalianza mwaka 1967 kwa
kushirikisha timu za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, na mwaka huu ni
mashindano ya 40 tangu kuanza kwa michuano hiyo
Klabu ya Simba ndio timu
inayoongzoa kwa kutwaa ubingwa huo mara sita (6) ikifuatiwa na Yanga, Gor Mahia
zilizotwa mara (5), APR ya Rwanda ikiwa imetwaa ubingwa huo mara tatu (3).
Yanga na Gor Mahia zina nafasi ya kufikia Simba SC endapo zitafanikiwa kutwaa
Ubingwa msimu huu.
Mechi ya ufunguzi ufunguzi
siku ya jumamosi uwanja wa Taifa itawaktanisha APR ya Rwanda dhidi ya Al Shandy
ya Sudan saa 8 kamili mchana, KMKM kutoka Visiwani Zanzibar watacheza dhidi ya
Telecom ya Djibout uwanja wa Karume saa
10 jioni, huku wenyeji timu ya Yanga wakiwakaribisha Gor Mahia kutoka Kenya saa
10 jioni.
Kuelekea kwenye mashindano
hayo, waandaji wa michuano hiyo CECAFA kwa kushirikiana na wenyeji Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya michezo hiyo, ambapo
Uwanja wa Karume kiingilio kitakua shilingi elfu mbili (2,000) na uwanja wa
Taifa kiingilio cha chini kitakua ni shilingi elfu tano (5,000) na kiingilio
cha juu ni elfu 20,000 (20,000).
Timu zinazoshiriki michuano
hiyo
Kundi A: Yanga (Tanzania
Bara), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar), Khartoum-N
(Sudan).
Kundi B: APR (Rwanda),
Al-Shandy (Sudan),LLB AFC (Burundi), Heegan
FC (Somalia).
Kundi C: Azam FC (Tanzania),
Malakia (Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia) na KCCA (Uganda).
Michuano hiyo ya CECAFA
Kagame Cup itaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha Supersport.
UCHAGUZI
TWFA
Kamati ya Uchaguzi ya Chama
cha Soka cha Wanawake chini (TWFA) inatangaza kuwa wafuatao wamepita katika
mchujo wa awali katika nafasi walizoomba kama ifuatavyo:
1.
Amina Ali Karuma -
Mwenyekiti
2.
Devotha John Marwa – Mwenyekiti
3.
Cecilia Makafu – Katibu Msaidizi
4.
Somoe Roberst Ng’itu – Katibu Msaidizi
5.
Debora Ernest Mkemwa – Mjumbe Kamati ya Utendaji
6.
Mwanaheri Kalolo – Mjumbe Kamati ya Utendaji
7.
Theresia Reginald – Mjumbe Kaamti ya Utendaji
Hivyo mtu yeyote mwenye
pingamizi anaombwa aliwasilishe katika ofisi za TFF – Karume kuanzia tarehe 15/07/2015 mpaka 20/07/2015.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment