Na Bryceson Mathias, Kibundu
MAGAIDI waliojificha
ndani ya Msitu wa Kata ya Kibindu, mpakani mwa Bagamoyo, Kilindi na Mvomero,
kwa sasa wanaathirika na Njaa, jambo ambalo linawafanya wang’oke msituni
walikojificha na kwenda kwenye Makazi ya Wananchi kujipatia Chakula kunusuru
Maisha yao.
Hatua ya Magaidi hao
kuathiriwa na Njaa, inatokana na Wananchi kwenye Migahawa ya Mama Lishe na Baba
Lishe, kutowauzia Chakula au Vitafunio watu ambao hawawatambui kama ambavyo
awali kwa kutojua, walikuwa wanawauzia Maandazi yalikuwa yakikusanywa hadi kufika
Gunia.
Wakati Magaidi hao wakihangaishwa
na Njaa msituni humo, pia zipo taarifa za Kamati Tatu za Ulinzi za Wilaya
Jirani kufanya Kikao cha Ujirani Mwema cha Wilaya Jirani, Mvomero, Bagamoyo na
Kilindi, ili kupanga Mikakati thabiti ya kuwadhibiti Magaidi hao wakishirikiana
na Wananchi.
Mmoja wa Viongozi wa
Kamati hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini kutokana na Kikao
hicho kuwa ni cha Siri alisema, ”Ni kweli kuna Kikao cha Ujirani Mwema wa
Kamati Tatu za Ulinzi na Usalama, za Mvomero, Bagamoyo na Kilindi, lakini
yanayojiri ni Siri hayasemwi.
“Tunawataka
Wanaowafadhiri na kuthubutu Kuwaficha Magaidi hao majumbani mwao, ambao ni
Vijana Wadogo wadodo, Watoe taarifa Polisi au kwa Viongozi wa Vijiji, na
ikibidi Magaidi wenyewe, Wajisalimishe wenyewe mapema, kabla hawajakumbana na Vyombo
wa Dola”alisema Mtoa habari.
Habari Mseto Blog lilimtafuta Mtendaji wa Kijiji cha Kibindu, Juma Mgaza, kwenye simu ili kujua
hali ya Usalama tuka kwenye Kijiji chake, lakini alijibu kwa Maneno ya Mkato,
na kusema, “Samahani niko kwenye Kikao”.
Hata hivyo, alipotafutwa
aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo, Mawazo Mkufya, kujua hali ya Ugaidi ikoje katika
Kata ya Kibindu alisema, “Ni kweli Adui yako Muombee Njaa! Hali sasa ni Shwali,
hapa tuna Askari wanaolinda Usalama na kupokea taarifa mbalimbali toka kwa
Wananchi kuwahusu Magaidi hao, lakini hatubweteki, tuko Ki-Ulinzi zaidi”.alisema
Mkufya.
Kwa Upande wake Mtendaji
wa Kitongoji cha Pera, Mwanahawa Mabwani, alipoulizwa hali kwake ikoje alisema,
“Pamoja na kwamba hali kwa sasa ni shwali, anakamatwa mtu mmoja mmoja,“Nimeamua
kujiunga na Mafunzo ya Mgambo yanayoendelea hapa, ili niwe Mkakamavu”.alisema.
No comments:
Post a Comment